Serikali Kuandaa Kanuni Za Udhibiti Wa Bei Ya Dawa Na Vifaa Tiba
Serikali
ipo kwenye mchakato wa kuandaa kanuni za kudhibiti bei za dawa nchini na tayari
rasimu ya kanuni hizo zimeshawasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel alipokuwa
akijibu swali lilioulizwa na Mheshimiwa. Mhandisi Mwanaisha Ng’anzi Ulenge
(Mbunge Viti Maalum) Bungeni, Jijini Dodoma.
Mhe. Ulenge amehoji Serikali ina mpango gani wa kutoa bei elekezi ya vifaa vya
tiba haswa akilenga vya macho, pua na koo.
Akijibu Kuhusu Vifaa tiba, Dkt. Mollel amesema kuwa bei elekezi za vifaa tiba
zitaandaliwa mara tu baada ya kukamilika kwa kanuni za bei elekezi za dawa.
No comments
Post a Comment