Ruvuma: Mke amkata mmewe sehemu za siri kwa wembe
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Hellen Mchahuru (40) kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumkata na wembe sehemu za siri (Korodani ya kushoto) mumewe Vintan Luhiva (42).
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Joseph Konyo amesema mtuhumiwa aliweza kufanya tukio hilo wakati mwanaume huyo akiwa amesinzia.
Ameeleza kuwa mtuhumiwa alichukua wembe na kumjeruhi kwa kumkata korodani moja upande wa kushoto na kumsababishia maumivu makali.
Kamanda Konyo amesema
majeruhi amelazwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Tunduru akipatiwa matibabu na
kwamba mtuhumiwa anayedaiwa kutenda tukio hilo yupo mikononi mwa jeshi la Polisi
na hatua za kumpeleka Mahakamani zinafuata baada ya hatua za upelelezi.
Related Posts
-
Next
Serikali Kuandaa Kanuni Za Udhibiti Wa Bei Ya Dawa Na Vifaa Tiba
-
Previous
Mwanamke mwingine auawa jijini mwanza:adaiwa kuchomwa kisu kisha kunyongwa na mzazi mwenzie
No comments
Post a Comment