Mbunge wa CCM Aibuka Katika Mkutano wa ACT-Wazalendo.....Polisi Wamwondoa Kuepusha Vurugu
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), aliyemaliza muda wake, Ally Keissy jana aliibuka kwenye mkutano wa kampeni wa chama cha ACT-Wazalendo na kupinga maelezo kwamba mshahara wake wa ubunge ni zaidi ya Sh10 milioni.
Keissy
aliwasili kwenye mkutano huo uliokuwa wa mgombea urais wa
ACT-Wazalendo, Anna Mghwira na mgombea mwenza wake, Hamad Yusuph Mussa
uliofanyika Kijiji cha Namanyere, akiwa kwenye gari lake aina ya Toyota
Land Cruiser.
Mgombea
mwenza, Mussa alipopanda jukwaani, alianza kuhutubia kwa kuwaeleza
wananchi kwamba mbunge wao, Keissy anayemaliza muda wake ameshindwa
kuwaletea maendeleo, hivyo mwaka huu wasimpe kura zao.
“Niwaambie
kitu, wabunge wenu akiwamo Keissy wanapata mshahara wa zaidi Sh10
milioni ndiyo maana akiwa bungeni kazi yake ni kupiga makofi kwa
kushangalia kupitisha kwa bajeti ambayo haina masilahi kwa wananchi wa
jimbo lenu,” alisema Mussa na kushangiliwa na umati ambao mmoja alisikika akisema:
“Sema baba sema, ujumbe umefika na mwenyewe yupo hapa.”
Kauli
hiyo ilionekana kumkera Keissy, ambaye alinyanyuka alipokuwa ameketi na
kwenda kwenye gari lake kuchukua ‘salary slip’ iliyogongwa muhuri wa
Ofisi ya Bunge, ikionyesha kwa mwezi anapokea mshahara Sh3 milioni.
Akionyesha
kukerwa na alichoeleza kuwa ni upotoshaji wa mgombea mwenza, Keissy
alikwenda karibu na meza kuu na kumwita Ofisa Habari wa ACT-Wazalendo,
Abdallah Khamis na kumkabidhi nyaraka hiyo ili aipeleke jukwaani kwa
mgombea mwenza aliyekuwa akiendelea kuhutubia.
Hata hivyo, Mussa alipopelekewa nyaraka hiyo aliwaambia wananchi: “Keissy anasema nimpige kidogo kidogo maana yamemchoma.”
Keissy hakuonyesha kuridhika na majibu hayo na alionyesha ishara za kutaka kulazimisha nyaraka hiyo isomwe, kitendo kilichozuiwa na askari waliokuwa eneo hilo na kumtaka aondoke kwa kuwa mkutano huo ulikuwa haumhusu.
Keissy hakuonyesha kuridhika na majibu hayo na alionyesha ishara za kutaka kulazimisha nyaraka hiyo isomwe, kitendo kilichozuiwa na askari waliokuwa eneo hilo na kumtaka aondoke kwa kuwa mkutano huo ulikuwa haumhusu.
Awali, Keissy aliwaambia waandishi wa habari kuwa: “Uchaguzi
wa mwaka huu ni mgumu kwa vyama vyote kutokana na uelewa na mwamko wa
wananchi, hivyo siyo vibaya hata mimi kuhudhuria mkutano huu.
“Hakatazwi
mtu kuhudhuria mikutano kama hii maana uchaguzi wa mwaka huu ni tofauti
na miaka mingine na ACT-Wazalendo wana siasa nzuri na kitakuwa chama
cha pili cha upinzani.”
Katika
mkutano huo, Mghwira aliwaambia wananchi waliohudhuria kwamba viongozi
waliopewa dhamana ya kuongoza nchi hawana cha kujitetea kuhusu kusuasua
kwa maendeleo nchini.
Alisema
katika mikoa aliyotembelea, ameona jinsi gani Watanzania walivyopigika
na ugumu wa maisha na hali hiyo inasababishwa na viongozi waliowapa
dhamana ya kuwaongoza kutojali maendeleo yao.
“Suluhisho
pekee la hali hii ni ACT-Wazalendo. Tumejipanga ipasavyo kuwatumikia na
endapo nikifanikiwa kuingia madarakani uchumi wa Taifa hili na thamani
ya shilingi haitoshuka ili kuleta maendeleo kwenu,” alisema Mghwira.
Pia,
aliwaahidi wakazi wa Katavi kubadilisha mfumo wao wa kilimo na kuwa
kilimo cha biashara ili vijana wake wapate ajira na kuachana na kilimo
cha kizamani na kuweka mfumo bora wa usambazaji wa pembejeo za kilimo.
Mpekuzi blog
No comments
Post a Comment