Header Ads

Header ADS

AFISA MTENDAJI WA KATA YA KITISI BWANA FUTE AMEWATAKA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO ILIKUENDELEZA MAENDELEO YA KATA HIYO

          Mtendaji huyo ameyasema hayo wakati wa utambulisho kwa wananchi kwani yeye ni mgeni ndo anaanza kazi.pia amewatakawananchi kufanya usafi katikamaeneo yanayowazunguka nakilamtuatakaye tupa taka ovyo faini ni sh,50000/=.
         Pia Diwani wa Kata hiyo mheshimiwa Nevy Sanga amewataka walimu wa shule zilizopo kwenye kata yake kuacha mapema tabia  ya kuwachangisha wazazi michango lasivyo mwalimu atakaye kaidi awetayari kuacha kazi.
          Kwa upande mwingine amemtaka mkuu wa shule ya msingi Kahawa kuwarudishia wananchi fedha alizochangisha kwa wazazi sh 5000/= kama michango ya shule wakati mheshimiwa Raisi amesema elimu nibure.
        Mheshimiwa Diwani amewataka pia walimu walio zoea kuweka tution mashuleni kuacha kabisa na badalayake wakafundishie nje ya majengo ya shule
        Kwa upande wa wananchi wameitaka serikali kurekebisha sheria ya kudai ushuru kwa wafanyabiashara wadogowadogo  wa sh 6000/= kwa mwezi na baadala yake watendaji wapite kwa kila siku watakapo ona vibanda vimefunguliwa wachukue mchango wa sh 200 kwa siku  kama atafungua basi mtendaji anawezakupitia kesho yake.

No comments

Powered by Blogger.