Header Ads

Header ADS

Wakuu wa Wilaya na Mkoa wapewa rungu la kutumbua watumishi

         Waziri wa nchi ,ofisi ya Raisi na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George  Simbachawene amesema kuwa  wakuu wa  mikoa na wilaya  wanafanyakazi  kwa mujibu wa sheria za jamhuri ya muungano wa Tanzania.















                Simbachawene ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali  la nyongeza la mbunge wa jimbo la chemba ,Juma Nkamia  kuhusu wakuu wa wilaya na mikoa  kuwa wababe katika maeneo yao ya kazi.
              Wakuu wa Mikoa na Wilaya  wanasimamia maeneo yao kwa mjibu sheria na wanahaki kuwachukuliahatua watumishi ambao hawatekelezi majukumu waliopewa,Alisema Simbachawene
              Aliendelea kwa kusema kuwa hata kama kuna wakuu wa ,mikoa na wilaya ambao ni wababe katika maeneo yao  ya kazi hauwezi kusema kila mkuu wa mkoa au wilaya aliyechukuahatuadhidi ya mtumishi ambaye hawajibiki katika kazi yake ni mbabe au muonevu
              Aidha Simbachawene alisema`kuwa ni wakati sasa watumishi wa umma kutekeleza  wajibu wao na kuacha kufanya kazi kimazoea kwani hakuna kiongozi atakaye weza kumchukulia hatua mtumishi ambaye anawajibika  na kazi zake kama alivyopangiwa.
            Vilevile alisemakuwa wakuu hao wa mikoa na wilaya wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika maeneo wanayoyasimamia kutokana na watumishi wengi wa serikali  waalikuwa wamejisahau kutekeleza wajibu wao na kufanya kazi kimazoea.

No comments

Powered by Blogger.