Gabon yasema imezima jaribio la kupindua Serikali ya Alli Bongo ambaye yuko Morocco.
Serikali Gabon yasema imezima jaribio la kupindua serikali ya Ali Bongo ambaye yuko Morocco
Hali ya kisiasa nchini Gabon "ni
shuwari na salama" msemaji wa serikali amesema baada ya wanajeshi
waaminifu kwa serikali ya Rais Ali Bongo kufanikiwa kuzima jaribio la
mapinduzi ya serikali nchini humo.
Tayari wanajeshi wote watano
waliohusika katika mapinduzi hayo wamekamatwa na mamlaka. Wanajeshi
wanne walikamatwa mapema wakati watano alisakwa kwa muda kabla ya
kufumwa akijificha chini ya uvungu wa kitanda.Msemaji wa serikali Bw Guy-Bertrand Mapangou ameambia BBC kwamba hali imerejea kuwa shwari.
"Hali ni tulivu. Polisi ambao huwa hapo wamerejea na kuchukua udhibiti wa eneo lote la makao makuu ya mashirika ya redio na runinga, kwa hivyo kila kitu kimerejea kawaida," amesema.
Kundi la wanajeshi nchini Gabon lilikuwa limetangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi na kutangaza amri ya kutotoka nje.
Wanajeshi wenye vifaru na magari ya kivita walikuwa wakishika doria katika barabara za mji mkuu Libreville.
Tangazo kutoka kwa kundi la vijana wa umri wa makamo lilitangazwa na kurudiwa katika kituo cha redio cha serikali nchini humo, ambapo wanasema kumekuwepo na wasiwasi kuhusu uwezo wa Rais Ali Bongo kuongoza nchi hiyo.
No comments
Post a Comment