Header Ads

Header ADS

Kuadimika kwa kondomu Njombe kwa tishia kuongezeka kwa maambukizi ya Ukimwi.



KondomuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mipira ya kiume ya kondomu nchini Tanzania imeadimika ama kupanda bei katika baadhi ya sehemu hususani mkoa wa Njombe ambao maambukizi ya Virusi vya Ukimwi yapo juu.
Hali hiyo imetokana na mabadiliko katika mifumo ya usambazaji wa mipira hiyo. Awali, serikali pamoja na baadhi ya mashirika binafsi nchini Tanzania yalikuwa yakipata ruzuku kutoka kwa taasisi ya Afya ya Global Fund.
Lakini sasa, ruzuku hiyo wanapatiwa serikali pekee, hii inamaanisha Wizara ya Afya  ndiyo itakuwa inasimamia uingizwaji wa kondomu kwa mpango huo.
Naibu Waziri wa Afya Tanzania Dkt Faustine Ndugulile ameiambia BBC Swahili kuwa kwa sasa mfumo huo upo kwenye kipindi cha mpito na matokeo yake ni kuwa baadhi ya maeneo hususani mkoa wa Njombe yameathirika vibaya.
Hata hivyo amesema si kweli kuwa hakuna kabisa kondomu katika maeneo hayo.
"Bado kuna mashirika mengine ambayo si ya kiserikali yanaingiza komdomu kwa mifumo yao binafsi na kuna zile ambazo zinaingizwa kupitia wafanyabiashara.

KondomuHaki miliki ya pichaISTOCK

"Kondomu zilizoadimika ni zile ambazo zilikuwa zikitolewa bure ama kwa bei nafuu. Na hili ni suala la mpito tu, karibuni mambo yatakuwa sawa kama awali."
Kutokana na uhaba huo, bei za kondomu mkoani Njombe zimepaa kwa kasi.
Gazeti la Mwananchi la Tanzania linaripoti kuwa bei ya pakiti iliyokuwa ikiuzwa kwa shilingi 5,000 ($2.14) sasa imefika 12,500 ($5.36).
Mwanaharakati wa kupambana na maambukizi mkoani humo Michael Uhahula ameiambia BBC kuwa bei za rejareja zimepanda kutoka wastani wa shilingi 500-1000 ($0.21-$0.43) mpaka shilingi 1,500-2,500 ($0.64-$1.7) kulingana na sampuli.
Wakati wastani wa kasi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa Tanzania inaripotiwa kuwa asilimia 4.5, kwa mkoa wa Njombe wastani wa maambukizi ni asilimia 14.
Itakumbukwa kuwa Mkoa  wa Njombe uliopo kusini mwa Tanzania ndio unaongoza kwa maambukizi ya Ukimwi Tanzania, na uhaba huo unaleta hofu ya tatizo kuongezeka.

No comments

Powered by Blogger.