kutokana na mauaji ya kimbari nchini Rwanda mayatima watafuta family zao.
Miaka 25 baada ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda, baadhi ya yatima kwa shauku kubwa wanaendelea kutafuta historia yao ambayo ilipotea.
Oswald hajui chochote kuhusu maisha yake kabla ya kuokotwa na mwanamke mmoja akiwa kwenye rundo la miili jijini Kigali, akijaribu kunyonya matiti ya mwanamke aliyepoteza maisha.
Inakadiriwa alikua na umri wa miezi kati ya miwili na mitatu, hakuna anayejua kwa hakika.
Kwa uhakika ni kuwa ni mmoja wa watoto wengi waliopoteza majina yao, miaka ya kuzaliwa na historia zao wakati wa siku 100 za machafuko yaliyoikumba Rwanda, yaliyoanza tarehe 7 mwezi Aprili, miaka 25 iliyopita.
Wakati Rwanda ikiadhimisha kumbukumbu ya mauaji hayo, Oswald na vijana wengine wa kiume na wakike kama yeye wamejikuta peke yao, wadogo sana kuweza kukumbuka maisha yao ya zamani, wamekua wakiangalia watu waliokusanyika wakijiuliza kama familia zao zitakua zimesimama miongoni mwa watu walionusurika, au ni miongoni mwa watu 800,000 wahutu na watutsi waliopoteza maisha.
''Kwa asilimia hamsini nafikiri wazazi wangu walifariki, asilimia 50 nina matumaini kuwa nitawapata,'' Oswald alisema, akionyesha matumaini ambayo yanaonekana kushangaza baada ya miaka mingi kupita.
Oswald ni miongoni mwa watoto 95,000 wanaoaminika kuwa yatima kutokana na mauaji ya kimbari, ambayo yalianza saa kadhaa baada ya ndege iliyokua imembeba rais wa wakati huo Juvenal Habyarimana kushambuliwa, kuanguka tukio lililogharimu maisha ya kila mtu aliyekua kwenye ndege hiyo.
Kuna kitu kimepungua
Mwanamke mmoja wa kabila la Hutu aliyemuokota, Josephine, alimpoteza mumewe wakati wa mauaji ya kimbari.Aliuawa na wanamgambo wakati akijaribu kuwasaidia watutsi
Alipitia madhila ya kubakwa na wanamgambo wa Interhamwe ambao walitekeleza mauaji dhidi ya watu wengi, kisha akaambukiwa virusi vya ukimwi.
Pamoja na shida hiyo, aliweza si tu kumtunza Oswald, lakini pia watoto wengine, akawatunza kama wakwake.
Lakini kadiri Oswald alipokua akikua, alianza kuhisi kuwa kuna kitu kimekosekana.
''Niliwaona watoto wengine na baba zao, na nikaanza kufikiria kuhusu wazazi wangu'', aliiambia BBC.
Kujaribu kujua wewe ni nani wakati unacho kidogo kukufanya usonge mbele ni vigumu sana
Kwa Jean Pierre, kutafuta kwake majibu kumefanyika kwa kutambua nyuso mitaani
''Nikimuona mtu anayefanana na mimi, ninahisi ni ndugu yangu,'' anasema Jean Pierre ambaye anaamini ana umri wa miaka 26 japo hana uhakika.
Njia hii, anaamini, inaweza kuzaa matunda: hivi karibuni alikutana na mwanamke mmoja anayefanana naye, kisha akamfuata ili aweze kumjua vizuri.
Ikabainika kuwa mwanamke huyo alipoteza kaka yake wakati huo, kijana mdogo ambaye kwa sasa angekua na umri sawa na Jean Pierre.
Jean Pierre alikimbia kwenda kukutana na mama.
Kusaidiana
''Nilipokutana na Mama Asalia, niliguswa,'' alisema.''Nilihisi ni mama yangu kabla hajatambulishwa kwangu.''
Wawili hao huwa wanawasiliana karibu kila siku, ingawa hawana ushahidi kuwa wana undugu, Vipimo vya vinasaba DNA ni ngumu kupatikana sababu ya gharama.
Lakini itakuwaje kama siye? akionyesha mashaka.Ataweza kuishi , hata hivyo ameishi miaka 25 imepita.
Oswald na Jean Pierre, na rafiki yao Ibrahim, waliamua kufanya jambo.Hivyo waliunda kundi kwa ajili ya kuwasaidia yatima wenzao.
Ibrahim amewasikiliza marafiki zake wawili wakisimulia.Kama wao, hafahamu ana umri gani hasa;Labda 25, anahisi.
Hajui majina ya wazazi wake-Kitu ambacho huwa anakumbushwa kila mara anapojaza fomu za kiofisi.
Si kama Oswald na Jean Pierre, haamini kama wazazi wake wako hai kutokana na namna alivyookotwa akiwa mdhaifu sana.
Wakati fulani ilikua karibu aipate familia yake:Miaka michache iliyopita,alialikwa kukutana na familia ambazo zilikua zikitafuta watoto wa kiume waliopotea wenye umri kama wake.
Ikaishia kuwa kumbukumbu mbaya kwake,yenye kuvunja moyo.
Hajakata tamaa, hana kazi na ndoto zake za kufika elimu ya juu ziliyeyuka.Anajiona mtu asiye na msaada, aliyetengwa, hisia ambazo marafiki zake wamezieleza pia.
''Hatuna msaada wa kutufanya tuweze kusonga mbele,'' Jean Pierre anaeleza. ''Hatuna namna ya kutufanya tuishi maisha mazuri.''
Walichonacho ni urafiki wao, na kupitia umoja wao 'Tumaini kwa familia ijayo' wamekubaliana kushirikiana kwa kila walichonacho.
Wakati tunaondoka, kuna swali moja la kuuliza linalokwenda kwa Oswald: Josephine, mwanamama aliyemlea kwa mapenzi atajisikiaje akijua kuwa ameipata familia yake?
Anatabasamu
''Itakuwa jambo jema kwetu sote.''
No comments
Post a Comment