Header Ads

Header ADS

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kufoji vyeti.

    Katika zoezi la usaili wa nafasi za kujiunga na JKT. Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linawashikilia vijana  sita kwa tuhuma za kufoji Vyeti.
    Akizungumza na Waandishi wa habari  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka  ,ambaye Pia ni Mwenyekiti   wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Njombe  amesema kuwa kutonkana na vitendo  vya udanganyifu ikiwemo kughushi vyeti vya uraia  wajumbe wa kamati hiyo wametengua  nafasi za uteuzi wa  Vijana  walioteuliwa kujiunga  na Jeshi la kujenga Taifa  na kusitisha zoezi la usaili na kupanga upya  maombi ya kujiunga na nafasi hizo.
      Baada ya kupitia Wilaya moja na nyingine tumebaini kuwepo kwa udanganyifu wa kuanzia vyeti vya kuzaliwa hadi vya elimu ya Msing  na tumegundua hata wengine uraia wao ni wa mashaka.tumesitisha zoezi baada ya kujiridhisha kuwa taarifa zilizowasilishwa mbele yetu baadhi   zinaudanganyifu mkubwa  sasa tumetangaza  upya vijana watume maombi  upya kuanzia tarehe 29 mwezi 6-  2019 mpaka tarehe 08 mwezi wa 07- 2019  .Vijana hawa watapaswa kuwasilisha maombi yao kwa wakuu wa Wilaya  kila mmoja kwenye Wilaya anayotoka' Amesema Ole Sendeka"    
   










No comments

Powered by Blogger.