Waziri Lugola awaka moto.
Waziri wa mambo ya ndani, Kangi Lugola amesema kuwa mpango wa Serikali ni kukemea vikali biashara haramu ya usafirishwaji binadam inayofanyika na baadhi ya wafanya biashara kwa dhumuni la kujipatia kipato .
Amesema hayo Jijin Dar es salaam,wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kudhibiti biashara ya binadam, ambapo amesema biashara hiyo kwa sasa ni sawa na biashara ya utumwa.
'' Biashara haramu ya usafirishaji wa binadam inayoongoza hapa nchini ni ya kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine ambapo waathirika zaidi ni watoto wadogo,wasichana na vijana ambao umri wao ni miaka 13 hadi 24 hali hii inadhihirisha wazi kwamba kuna utumwa licha ya utumwa ambao tulifanyiwa na wenzetu wakati ule, bado kuna baadhi yetu wanaowafanya watanzania wenzetu kuwa watumwa.''Amesema Kangi Lugola. Ikumbukwe kuwa siku ya kupinga biashara ya binadamu kimataifa huadhimishwa kila mwaka julai 30.

No comments
Post a Comment