Hasira kali yazuka Uingereza kutokana na kusitishwa kwa Vikao vya Bunge.
Kutokana na Waziri Mkuu kuamua kuzuia Bunge kumepelekea kutokea kwa Ghadhabu kubwa dhidi ya Wabunge pamoja na Wapinzani wanaopinga kuidhinishwa Brexit pasipokuwa na Mpangilio.
Maandamano makubwa yalipelekea kuzuka Nchini humo kutokana na hatua hiyo pia waraka uliosainiwa na zaidi ya watu miliono moja wakipinga hatua hiyo,hata hivo pia kesi iliyowasilishwa dhidi ya hatua hiyo.
kwa mujibu wa Serikali nchini humo imeeleza kuwa kuistishwa kwa wiki tano ya vikao vya Bunge mwezi September na Oktoba kutakuwa na muda mwingi wa kujadili kuhusu Brexit.
Hata hivyo, kwa upande wao wakosoaji wamedai kuwa ni hatua''Isiyo ya Kidemokrasia''kuwazuia Wabunge kupinga Brexit bila ya mpangilio.
Akizungumza na BBC waziri Michael Gove ameeleza kuwa kutokana na kuidhinisha kwa Malkia kusitishwa kwa Bunge siku ya jumatano'bila shaka sio, hatua ya kisiasa kuzuia upinzani kwa hatua ya Uingereza kujitoa katika muungano wa Ulaya bila kuwepo na makubaliano husika.
Aidha ameendelea kueleza kwamba kutakuwa na ''Muda mwingi''kabla ya muda ulioorodheshwa wa kuondoka ifikapo Oktoba 31 wa kuweza kujadili kuhusu Brexit.
Ifikapo Oktoba 14,hotuba ya malkia itatolewa baada ya kusitishwa Vikao vya Bunge na kueleza ajenda yake ya kusisimu ,hayo yamesemwa hapo jana jumatano na Bwana Johnson.
Lakini pia amesema kuwa kabla ya kuendelea na mipango ya kuisogeza nchi mbele,hataki kusubiri Maka baada ya Brexit.
Kwa mujibu wa Jacob Rees Mogg,ambaye ni Kiongozi wa Bunge nchini humo aliyeweza kuudhuria katika mkutano wa Malkia, ameeleza kwamba vikao hivyo vya Bunge vilikuwa ni virefu kuwahi kushuhudia katika takribani ya muda wa miaka 400,hiyvo basi kusitishwa na kuanza upya ni sawa tu.
Jeremy Corbyn ambaye ni kiongozi wa chama cha Leba amezungumzia hatua hiyo ni kama ''pigo na unyakuzi wa Kidemokrasia yetu''kuweza kulazimisha Brexit pasipo kuweka makubaliano halali na mpangilio kwa kuwaacha wabunge pasipokutimia muda wao wa kupitisha Sheria bungeni.Hatua hiyo ya kusitishwa bunge aliahidi kujaribu kusitisha.
Kutokana na uamuzi huyo wa Johnson mwanaharakati Gina Miller ambaye anapinga Brexit lakini pia ndiye aliyewahi kushenda kesi ya Mawaziri kuhusu kipengere cha 'Article 50'amepeleka ombi la kuikagua sheria dhidi ya uamuzi huo.
Ifikapo mwishoni mwa Oktoba Waziri Mkuu huyo ameeleza kwamba anaitaji kutoka kwenye Umoja wa Ulaya huku pakiwepo na mpangilio lakini hata hivo amesema yuko radhi kuondoka hata pasipokuwepo na mpangilio.
Waandamanaji walikusanyika Westeminster hapo jana jumatano jioni,huku wakiwa wamebeba mabango na kupiga kelele wakisema''Sitisha Mapinduzi''huku wakipinga kujitoa katika Umoja wa Ulaya wakiwa wamebeba na Bendera za Muungano huo.

No comments
Post a Comment