Header Ads

Header ADS

Marais wastaafu wahudhuria Mkutano wa SADC

Marais wastaafu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wamehudhuria Mkutano mkuu wa 39 wa SADC unaoendelea katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa Julius Nyerere uliopo Dar es salaam kuona jinsi Rais wa awamu ya tano,Dkt John Pombe Magufuli akipewa uenyekiti wa Jumuiya hiyo.
  Hata hivo miongoni mwa marais waliohudhuria ni pamoja na Ally Hassan Mwinyi Rais wa Serikali ya awamu ya pili,Benjamin Mkapa rais wa Serikali ya awamu ya tatu,Jakaya Kikwete rais wa awamu ya nne pamoja na Rais mstaafu wa Serikali ya Zanzibar Aman Karume.













Licha ya wastaafu hao kuwepo katika mkutano huo na kutambulishwa kwa wageni mbalimbali kutoka nchi kumi na tano ya jumuiya ya SADC,Pia walikuwepo viongozi wengine wa Serikali ya Tanzania waliohudhuria ambao ni  Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt Mohamed Shein.
  Pia wengineo ni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Balozi John Kijazi,Mawaziri,Viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
 Kwa sasa nafasi hiyo amepewa Dkt John Pombe Magufuli,ambapo kwa mara ya mwisho ilishikiriwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa miaka 16 iliyopita.

No comments

Powered by Blogger.