Header Ads

Header ADS

Msafara wa Mkuu wa Wilaya washambuliwa kwa mawe

    Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi imeeleza kuwa Claudia Kitta ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kyela,pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya  katika msafara wake uliolenga kwenda kumuokoa mama mmoja aliyekuwa akipigwa na wananchi wakimtuhumu kwamba amemuua mwanaye wa kumzaa msafara huo ulishambuliwa kwa mawe.
   Hata hivyo amesema kuwa kutokana na kufariki mtu huyo katika uwanja wa mpira,ilipelekea wananchi wa wilaya hiyo kupatwa na wasiwasi na imani za kishirikina ya kuwa mama yake mzazi ndiye aliye muua na hivyo basi  muda wa mazishi ulipofika wakagoma kuzika maiti na kudai kwamba mama yake ahifufue maiti hiyo.













  Dc Claudia pamoja na kamati yake ya Ulinzi naUsalama walikuwa wakiendelea na ukaguzi wa Mwenge na Mitihani,ndipo taarifa kuhusu mama huyo zilipowafikia na kuamua kujiridhisha kuhusu taarifa hizo kwa kupitia eneo la tukio ndipo wananchi walipofunga njia na kuibuka kwa vurugu.
    Aidha,kwa mujibu wa kamanda wa Polisi ameeleza kuwa vurugu hiyo ilikuwa kubwa lakini hakuna mtu aliyelazwa hata hivyo waliokuwa katika msafara huo walijitaidi kutetea maisha yao pia Polisi kuwasiri mapema katika maeneo ya tukio na hata hivyo baadhi ya Polisi bado wapo katika sehemu ya tukio wakiendeleza na uchunguzi ili kuweza kuwabaini waliohusika na vurugu hiyo.

No comments

Powered by Blogger.