Bunge la jamuhuri ya Tanzania lapanga kuanza kidigitali zaidi
Kwa mujibu wa Job Ndugai ambaye ni spika wa Bunge la Tanzania limeweka mikakati ya kutumia mfumo wa kidigitali Bungeni kwa ajili ya kuwapa wabunge nyaraka mbalimbali na kuachana kabisa na mfumo wa sasa wa kutumia makaratasi na kuanza kuwawekea nyaraka hizo kupitia simu zao.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni jijini Didoma na Spika Ndugai wakati wa kikao cha kwanza cha mkutano wa 16,wa bunge la kwanza,ambapo ameeleza kuwa katika Afrika Mashariki bunge pekee ambalo lina tumia karatasi ni Tanzania pekee.
''Sisi ndiyo bunge pekee Afrika Mashariki ambao tunaendekeza makaratasi mengi,wenzetu hawatumii,tunaanza na hii'Order paper'halafu tutaenda kidogo kidogo.
''Mpaka tufikie hatua dawati la bunge liwe safi naombeni mhakiki simu zenu na barua pepe,tunaanza kuwapatia nyaraka,''Spika Ndugai amesema.
Mkutano wa bunge la 16 umeanza Jijini Dodoma leo September 3,2019,ambapo Miraji Mtaturu aliapishwa kuwa mbunge wa Singida Mashariki,akikalia kiti cha nafasi yaTundu Lissu

No comments
Post a Comment