Header Ads

Header ADS

Familia ya Mugabe yatofautiana na Serikali kuhusu mazishi.

       Familia ya aliyekuwa Raisi wa Zamani wa Zimbabwe Robart Mugabe yatofautiana na Serilikali ya Zimbabwe juu ya sehemu gani atakapozikwa kiongozi huyo wa Zamani.
The body of former Zimbabwean President Robert Mugabe arrives at the Blue Roof, his residence in Borrowdale, Harare, Zimbabwe, on 11 September 2019
    Itakumbukwa kuwa Mugabe alifariki dunia wiki iliyopita akiwa na umuri wa miaka 95 Singapore alipokuwa anapatiwa matibabu .
Familia yake inasema mwili wake utalazwa kuonekana mara ya mwisho nyumbani kwake katika kijiji cha Kutama Jumapili usiku, na atazikwa katika mazishi ya faragha.
"Mwili wake utapewa heshima za mwisho Kutama Jumapili usiku na kufuatwa na mazishi ya faragha - pengine Jumatatu au Jumanne - na sio katika makaburila ya kitaifa ya mashujaa wa uhuru. Huo ni uamuzi wa familia nzima," binamu yake, Leo Mugabe ameliambia shirika la habari la AFP.
Rais Emmerson Mnangagwa alimtangaza Mugabe kuwa shujaa wa kitaifa baada ya kifo chake, na kuashiria kuwa anapaswa kuzikwa katika eneo hilo la kitaifa.
Waziri wa elimu Paul Mavhima amesema hakuna shaka Mugabe anasathili kuzikwa kama shujaa wa kitaifa.
"Mtu muhimu wa aina hiyo, ambaye mazishi yake yatahudhuriwa na zaidi ya viongozi 50 wa taifa na wa zamani. Muasisi wa taifa hili hakupaswi kuwa na majadiliano ya hilo. hakupaswi kuwa na mzozo wowowte. Uamuzi unapaswa kuwa wa wazi, anastahili kuzikwa katika kaburi la kitaifa,"amesema
"Itakuwa ni makosa makubwa kuwa na mpiganiaji uhuru wa taifa hili, mhamasishaji mkubwa wa raia wa Zimbabwe kuzikwa katika eneo jingine lolote kando na kaburi la itaifa. Wito ni kuiomba familia - huyu sio wenu tena, ni kiongozi wa taifa. Ni kiongozi wa Afrika. Ni kiongozi duniani, Anastahili kupewa heshima anayoistahili . Kwahivyo atazikwa katika kaburi la kitaifa''

No comments

Powered by Blogger.