Header Ads

Header ADS

Mbowe ahoji kanuni za uchaguzi Serikali za Mitaa 2019

   Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo [Chadema] ambaye ipa ni kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni amehoji kama ni sahihi kwa kanuni za Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 kuanza kutumika kabla ya kamati  ya sheria ndogo kupitia .
      Mbowe amehoji swali hilo mara baada ya kupata nafasi ya kuuliza swali  la nyongeza  katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni jijini Dodoma.











        Amesema kuwa inawezekana watu wakaona mambo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni madogo lakini amani ya Nchi inaweza kupotea au kuathirika kama mambo hayo yasipopewa kipaumbele.
      Mbowe amehoji kuwa"Mheshimiwa Waziri atueleze katika utamaduni huo ambapo kanuni tayari zimeshaingizwa kazini huku kamati ndogo haikuzipitia kwa kizingizio ya kwamba wadau walizipitia jambo ambalo siyo kweli"Amehoji Mbowe.
      Pia kiongozi hoyo wa Kambi rasmi Bungeni ameongeza kwa kusema kuwa kamati ndogo ya Bunge haijawahi kupitia wala kuziona kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019

No comments

Powered by Blogger.