Header Ads

Header ADS

Muongozaji Watalii ajirusha na kufa mlima Kilimanjoro

     Thomas Meela (58), mkazi wa Marangu anayejishughulisha  kuongoza watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro amekufa baada ya kujirusha kwenye kilele cha mlima huo umbali wa mita 5,895.Akizungumza leo Jumanne Septemba 17 ,2019  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa  Kilimanjaro  Hamiss Issah , amesema tukio hilo limetokea Septemba 15,2019 katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

    "Alichanganyikiwa baada ya kupata homa ya Mlima na kuamua kujirusha na Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo"Amesema Kamanda wa Polisi.Kwa mujibu wa taarifa Muongozaiji wageni huyo alikuwa na safari ya siku tisa kupanda Mlima Kilimanjaro Septemba 12 ,2019 mchana baada ya kufika kileleni aliwaacha wageni na kwenda kuvuta sigara lakini akiwa na mwenzake ndipo alipomwambia kuwa hawatamwona tena''
     ''Mwenzake alikwenda kutoa taarifa kwa watu aliokuwa nao ili wampe msaada aliporudi walikuta  amekimbia na tayari ameshajirusha kilele cha uhuru na kuangukia miamba''amesema
   


No comments

Powered by Blogger.