Header Ads

Header ADS

Sababu za Maimai kuweka Silaha chini

    Kundi la wapiganaji wa Maimai Nchini Congo limekubaliana na wito uliotolewa na Raisi Felix Tshisekedi  kurudi katika maisha yao yakawaida au kuweka silaha chini na kujiunga na Jeshi la Nchi hiyo.
       Kundi la wapiganaji wa [UPCL] wamekusanyika katika mji mdogo wa Kulunguta kwa ajili ya kusalimisha silaha zao
       Bwanakawa Masumbuko Nyonyi ambaye ni Meya wa Mji wa Beni alieza kuwa kutokana na kauli ya raisi wa Nchi hiyo Felix Tshisekedi ya kuwataka wapiganaji hao mnamo mwezi Aprili mwaka huu kuachia silaha zao chini.
Wapiganaji nchini DR Congo
      Meya  uyo ameeleza kuwa wito huo umefwatia kwa mateso waliyopitia wakazi wa mji huo na viunga vyake licha ya mbinu mbali mbali za kuhimarisha Jeshi la Nchi hiyo ili kuweza kupambana na kundi la wapiganaji wa ADF, ndiyo wametajwa kuwa ni maadui wakubwa wa  Taifa na Serikali yao
.''Tangu rais wa DR Congo alipopita mjini Beni alitoa wito kwa wapiganaji wa Maimai kuweka chini silaha kutokana na mateso walioyapitia wakaazi wa mji huo kufuatia uvamizi wa mara kwa mara wa wanamgambo wa ADF, baadhi yao wamekubali wito huo'', alisema.
     Aidha amesema kuwa kundi dogo ambalo limekubali kuweka silaha chini ili kujumuika na ujenzi wa kulijenga nchi yao ambalo baadhi ya maeneo yakiwa yanakabiliwa na vita vya wao kwa wao na kwa kipindi cha mda mrefu.
     Pia Bwanakawa amesema kuwa baadhi ya waliyokubali watajumuishwa kwenye jeshi mbali na huduma nyingine za kitaifa huku wale wanaotaka kurudi nyumbani watahudumiwa na kurudishwa hadi makwao.
    ''Kila mtu ataulizwa aina ya kazi anayotaka kufanya au kujifunza iwapo ni ujasusi atapelekwa huko na kuna wale ambao watafunzwa kazi za mkono - kama huduma ya taifa. Kuna njia nyingi ambazo wakati watachukuliwa ''Tunajua kwamba wanamgambo wa majimaji hawakuwa wakifuata sheria za kimataifa kwamba hawafai kuwapatia watoto silaha, hivyobasi kuna watoto walio na umri wa hata miaka 15 waliopatiwa silaha ili kujumuika katika vita, kitu tutakachofanya ni kuwachukua na kuwakabidhi mashirika yasiokuwa ya kiserikali ili kuwasaidia kabla ya kuwarudhisha nyumbani kwao ili waridhike''
    Hata hivyo juhudi za Serikali ya Congo ni kuhakikisha wanasalia na adui mmoja ambaye ni wapiganaji wa kundi la ADF amesema Meya huyo.
    Pia ameeleza kwamba kwa wapignaji walio na umri na mdogo watawasilishwa katika mashirika yasiyo ya kiserikali ili kusaidia na baadaye watarudishwa nyumbani.
    
   

No comments

Powered by Blogger.