Header Ads

Header ADS

Tanzania kupitia usambazaji gesi asilia viwandani Serikali yapata mabilioni.

   Dkt.Medard Kalemani ambaye ni Waziri wa nishati Tanzania kupitia shirika la maendeleo ya petroli TPDC,inategemea kuvuna kati ya shiling milioni 85 hadi 120 kwa mwezi, sawa  na shilingi bilioni 1.02 hadi 1.4 kwa mwaka kutokana na matumizi ya gesi asilia katika kiwanda cha Lodhia kilichopo Mkuranga, ambayo hadi sasa ni futi za ujazo laki mbili kwa siku.
   Ambapo hayo yamezungumzwa mnamo septemba 24,2019 wakati Dkt.Medard Kalemani waziri wa nishati alipozindua matumizi ya gesi katika kiwanda hicho ambapo awali kilikuwa kikitumia mafuta mazito.















   Kufuatia makusanyo hayo kwa Serikali lakini pia kwa upande wa kiwanda hicho kimeweza kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa zake kwa zaidi ya asilimia 40 ukilinganisha na gharama zao za mwanzo zilizokuwa zikitumia katika kwa ajili ya mafuta mazito kutokana na matumizi ya gesi asilia.
     Akizungumza baada ya kukagua shughuli za kiwanda hicho pamoja na kufanya uzinduzi husika, Waziri alitoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) pamoja na wataalamu wa Wizara, kufanya mapitio ya bei za gesi viwandani ili ziwawezeshe wawekezaji kuzalisha kwa tija.
       “Mje na bei muafaka ambazo haziathiri uwekezaji wa TPDC na haziathiri uwekezaji wa wenye viwanda lakini pia zisiathiri mapato ya serikali,” Waziri alisisitiza.
     Aidha,Waziri aliendelea kufafanua zaidi kwa kusema kuwa bei ya sasa inaanzia Dola 4.7 hadi 7.72  kwa uniti moja,ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wawekezaji.
     Hata hivyo,Waziri aliiagiza TPDC na kampuni yake tanzu ya GASCO, kukamilisha zoezi la ukusanyaji takwimu kwa ajili ya usambazaji wa gesi wilayani Mkuranga ndani ya kipindi cha miezi miwili ili ziwezeshe kubaini mahitaji ya gesi viwandani katika wilaya hiyo na kuvisambazia nishati hiyo kwani umuhimu wake ni mkubwa.
     Lakini pia,Dkt Kalemani alisema kwamba baada ya Serikali kufanya mapitio ya bei za umeme itafanya marekebisho hususani baada ya kukamilika kwa miradi mikubwa ya uzalishaji wa umeme wa ikiwemo wa Julius Nyere-Rufiji  bei hizo zitapungua.
       Aidha, aliwataka wadau wa sekta za gesi na mafuta, kutoa ushirikiano wakati wa zoezi la kupitisha mabomba ya gesi katika maeneo yao. “Msidai fidia kwakuwa nasi hatutozi gharama za kuunganisha. Hivyo nanyi, msilete vikwazo.''
    Lakini pia, Waziri aliuagiza uongozi wa TANESCO wa Wilaya, Mkoa na Makao Makuu, kukipatia kiwanda cha Lodhia megawati nane zaidi za umeme kama kilivyoomba ili zifike 14 kufikia mwisho wa mwezi huu.
        Vilevile alieleza kwamba sababu ya kutekeleza kwa agizo hilo hakuna kwa sababu kuna umeme wa kutosha hata hivyo alisema kusiwe na mgao wa umeme wilayani humo kwani kuna umeme wa ziada.
    Aidha, Waziri aliitaka TANESCO kuhakikisha vijiji vyote 88 vya wilaya hiyo vinaunganishiwa umeme kupitia miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa.
    Filberto Sanga ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Mkuranga aliishukuru Serikali na kutoa pongezi katika Wizara ya nishati kwa jitiada za kusambaza nishati ya umeme na gesi kwa wananchi nchini.
       Lakini pia,kutokana na Wilaya yake kuwa na viwanda vingi aliomba Serikali itoe kipaumbele katika kupatiwa huduma hizo za umeme,Mkurugenzi Mtendaji wa Lodhia, Sailesh Pandit, alisema Wizara ya Nishati, kupitia TPDC na TANESCO imekuwa ikiwapa ushirikiano mkubwa
    Aliwaasa wamiliki wengine wa viwanda kujikita kwenye matumizi ya gesi asilia kwani inapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za uzalishaji,kutokana na kuongeza tija ya uzalishaji wao kutokana na Serikali kuwapatia nishati wanayoitaji pasipo kuwepo na vikwazo.
     Goodwill Ceramics kilichopo kijiji cha Njopeka ni miongoni mwa kiwanda kingine ambacho kimeunganishwa na gesi asilia huku hatua za kuunganisha wateja wengine zikiwa zinaendelea.


No comments

Powered by Blogger.