Header Ads

Header ADS

Ujenzi wa kumbi za starehe Iringa, Waziri mkuu asitisha.

   Kassim Majaliwa ambaye ni Waziri mkuu wa Tanzania ampa Mkurugenzi wa Manispa ya Iringa Hamid Njovu muda wa saa nne awe ameshaandika barua inayo lenga kusitishwa kwa ujenzi wa kumbe za sherehe pamoja na ukumbi wa mkutano katika eneo la shule ya msingi Gangilonga katikaa Manispa hiyo.
       Aidha,amemtaka Mkurugenzi huyo kusitisha mkataba na mtu aliyemkodishia eneo hili lakini pia kuzungushia uwigo katika eneo hilo kwa ajili ya matumizi ya shule,hata hivo amesema maeneo yote ya taasisi ya elimu nchini hayaruhusiwi kujengwa miradi ambayo haihusiani na masuala ya elimu.











  Hayo amezungumza mnamo Septemba 28,2019  wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Madiwani wa Halmashauri hizo akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya kikazi mkoani Iringa.
    “Mkurugenzi kafute mikataba yote ya ujenzi wa miradi katika eneo la shule ya Gangilonga pamoja na shule ya Wilolesi kwa sababu maeneo hayo hayaruhusiwi kujengwa miradi isiyohusiana na elimu. Eneo hilo lisafishwe na ujengwe uzio.”  Waziri amesema
  Lakini kwa upande wake Nocholous Mwasungura ambaye ni mwanasheria katika Manispa ya Iringa ameeleza kwamba aliandaa mkataba huo wa kupangisha eneo hilo kwa maelekezo ya kamati ya fedha,alisema hivo kutokana na Waziri mkuu kumuuliza ni kwa nini akuwashauri  kuhusu suala hilo kwa sababu tayari Serikali ilishatoa waraka wa kuzuia jambo hilo.
     Aidha, Waziri Mkuu amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happi ofisi ya ardhi ya Manispaa ya Iringa kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka wananchi juu ya Afisa Ardhi ambaye anadaiwa kujigawia viwanja vingi pamoja na kugawa kiwanja kimoja kwa mtu zaidi ya mmoja.
   Ambapo kabla Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Ally Happi alishatoa onyo kwa watumishi kujihusisha na matumizi mabaya ya madaraka yao pamoja na matumizi ya rushwa,roho mbaya,ubinafsi ikiwemo na chuki badala yake wafanye kazi kwa bidii pamoja na kushirikiana.
   Hata hivyo,Richard Kasesera aliwasilisha ombi kwa Serikali kuwa kutokana na magari mengi ya wilaya hiyo kuwa chakavu sana aliiomba Serikali iwanunulie vyombo vya usafiri kiasi kwamba Mkurugenzi asiwe anaomba rifti kwake.Na kwa mujibu wa Waziri mkuu kuwataka waombe kibali cha ununuzi wa Magari vilevile watumie pesa zao za ndani kwa ajili ya matumizi hayo.

No comments

Powered by Blogger.