Header Ads

Header ADS

UTPC.Yaiomba Serikali kupitia upya sheria ya huduma ya habari ya mwaka 2016

               Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari Tanzania [UTPC] umeiomba Serikali kutazama upya sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 na sheria ya mtandao kwani imekua kandamizi kwa waandishi.
             Hayo yamesemwa na Rais wa muungano wa vilabu vya uandishi wa habari Tanzania[UTPC] Deogratias Nsokolo katika hotuba yake kwenye  Mkutano mkuu wa UTPC  uliofanyika leo Visiwani Zanzibar.













                     Pia mkutano huo umehudhuriwa na Raisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif  Ali Idd Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Andres Sjoberg pia viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri.
          "Tunaomba Serikali ya Muungano kupitia Bunge ipitie upya sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 na sheria ya mtandao ambazo zimekuwa ni kikwazo kwa waandishi," amesema Nsokolo.Pia ameiomba Serikali kuwasaidia waandishi ambao wamekua wakikutana na hadha mbalimbali ikiwemo vipigo na manyanyaso na mateso kwenye maeneo yao ya kazi ili wafanye kazi zao kwa uhuru.
          


             




               

No comments

Powered by Blogger.