Atupwa Jela miaka Saba kwa kosa la kupoka Mtoto.
Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Njombe imemuhukumu miaka saba kwenda jela Joel Nziku kwa kosa la kupoka kwa nia ya kumficha mtoto Gaudence Kihombo (7) mkazi wa kijiji cha Ikando wilaya ya Njombe.
Akisoma hukumu ya shauri la jinai namba 44/2019,Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Njombe James Mhanusi, amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu namba 246 na kifungu namba 249 vifungu vyote vya kanuni ya adhabu sura 16 ya sheria kama ilivyofanyiwa marekebisho 2002, mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yake alikana na hivyo kusikilizwa katika mahakama zote mbili.
Pia Amesema Mahakama imezingatia kama alivyosema mwendesha mashtaka wa serikali kwamba makosa ya kupoka watoto ni makosa ambayo yanajitokeza sana katika mkoa wa Njombe na hivyo mahakama inapaswa kutoa adhabu kali.
‘’Lakini mahakama pia imeangalia kwamba mshtakiwa ni mara ya kwanza lakini mahakama imeangalia maombolezo yake hata hivyo pamoja na mambo yote makakama hii inapaswa itoe adhabu kali kwa kua makosa haya ya kupoka watoto yamekuwa ni makosa yanayojitokeza mara kwa mara hapa katika mkoa wa Njombe kwa hiyo mahakama inapaswa kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa mstakiwa na watu wengine’’.
‘’Hivyo basi shitaka hili la kupoka mtoto kwa nia ya kuficha adhabu yake ya mwisho kabisa ni miaka saba gerezani kwa hiyo mahakama inampatia mstakiwa adhabu ya mwisho, adhabu ya kifungo miaka saba gerezani na faili litaenda mahakama kuu kwa ajili ya kuthibitishwa adhabu’’alisema Mhanusi.
Awali Mhanusi alisema kwa upande wa mashtaka inadaiwa kwamba januari sita mwaka huu huko katika kijiji cha Ikando katika kata ya kichiwa wilaya ya Njombe mshatakiwa bila ya uhalali wowote alimpoka mtoto Gaudence Kihombo kwa nia ya kumficha
Hata hivyo alisema mshtakiwa kwenye utetezi wake alieleza jinsi alivyokamatwa kufikishwa kituo cha polisi Mkambako na kwenye utetezi wake alikataa kwamba yeye hakuwahi kufanya hilo tukio la kumpoka huyo mtoto lakini pia kwenye utetezi wake anasema hajawahi kuishi huko kijijini tangu alipoondoka akiwa mdogo lakini vile vile kwenye maelezo yake anasema hata nyumba yake baada ya kukamatwa ilivyoenda kupekuliwa hakukukutwa ushahidi wa aina yoyote hivyo alikanusha.
Upande wa mashtaka walileta mashahidi sita ambapo shahidi namba moja Rehema Kipakate bibi wa muhanga alikwenda kanisani na Gaudence Kihombo ambapo walipokua kanisani mtoto huyo alitoka na baadae kupitia shahidi namba tatu Joyce Kaduma ambaye ni mama mzazi wa shahidi namba tano Philipho Mwinami alimueleza shahidi namba moja ambaye ni bibi wa muhanga kwamba Gaudence alionekana akiwa na shahidi namba tano wakienda kuchunga ng’ombe katika msitu wa tanwat katika kuuliza uliza alionekana akiwa na Philipo Mwinami ambaye ni shahidi namba tano wakiwa wameenda kuchunga ng’ombe kwenye msitu wa tanwat.
“Bibi aliendelea kutafuta mjukuu wake na kutoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji sambamba na ndugu wengine hivyo basi mtoto huyo alianza kutafutwa bila ya mafanikio hata hivyo baadae uongozi wa kijiji uliamua kuiitisha kikao na kuanza kutafuta bila ya mafanikio yoyote lakini babu wa marehemu shahidi namba nne ambaye ni babu Gaudence Kihombo na watu wengine waliendelea kumtafuta lakini baadae kwa maelezo ya shahidi namba tatu,shahidi namba tano Philipo Mwinami alitoa maelezo ya kwamba yeye aliambiwa na mstakiwa wanapaswa kwenda kushunga ng’ombe akiwa na huyo Gaudence yaani akiwa na huyo mhanga siku hiyo ya tarehe sita na asipoenda na huyo muhanga kwenye msitu wa tanwat basi atakiona chamoto”walisema.
Shahidi huyo namba tano Philipo Mwinami aliiambia mahakama baada ya kutishiwa siku ya tukio ilibidi amtafute huyo Gaudence Kihombo ili aende nae kuchunga na baada ya kwenda machungani mshtakiwa alijitokeza na kumchukua mtoto na mwenzake alishindwa kutoa msaada kwa sababu walikua wawili na wote ni watoto.
Hata hivyo shahidi huyo namba tano aliieleza mahakama kuwa mstakiwa alimtishia kuwa asimwambie mtu yoyote na akimwambia mtu atakiona cha moto na hivyo akumueleza mtu mpaka baada ya kubanwa na hao mashahidi na ndipo alipoamua kueleza ukweli namna ambavyo mstakiwa alimkamata mtoto na kwenda nae kwenye gari yake na baadae kutokomea kusikojulikana hadi sasa mtoto huyo hajapatikana.
Mshtakiwa Nziku wakati wa kujitetea alisema anawatoto nane ambao wanamtegemea na amezaliwa peke yake pia Kuna shuguli nyingi za kumuingizia kipato ambazo hakuna mtu wa kuziendesha zaidi ya yeye mwenyewe.
Awali wakili wa serikali Nura Manja aliiambia Mahakama hiyo kwamba itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
Naye mama mzazi wa mtoto huyo Josephine Kihombo,aliishukuru mahakama kwa kutoa dhabu hiyo lakini bado hajajua hatima ya kupatikana kwa mtoto wake ambaye hadi sasa hajulikani yuko wapi.
Joel Nziku pia anatuhumiwa kwa kosa la mauaji ya watoto watatu wa familia moja yaliyotokea mapema Januari Maka huu mkoani Njombe.
No comments
Post a Comment