Fatma Karume aweka wazi Siri ya Mwl.Nyerere.
Hayo amezungumza mara baada ya Big Chawa wa Planet Bongo ya East Africa Radio kutembelea ofisini kwake ambapo ameeleza anaikumbuka sana picha ya Babu yake iliyopo Ofisini kwake Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, Mwl. Julius Kambarage Nyerere na aliyekuwa kiongozi wa Ethiopia, Haile Selassie.
Aidha,Fatma amesema kwamba Amesema anakumbuka mengi anapoiona picha hiyo, hasa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwani kipindi babu yake ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume amefariki, Mwl. Nyerere ndiye alikuwa ni kama babu yake aliyebakia.
"Naipenda sana picha hii (akiionesha) hapa ofisini kwangu, ninampenda sana babu yangu na huyu mbwa wa Haile Selassie hapa, lakini pia nampenda sana mwalimu kwa sababu pia alipofariki babu yangu, yeye alikuwa babu yangu aliyesalia", amesema Fatma huku akionesha picha hiyo.
Kutoka Octoba 14,1999 hadi sasa ni miaka 20 tangu kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kilichotokea.
No comments
Post a Comment