Header Ads

Header ADS

Halmashauri zaweka mikakati ya kutokomeza mazalia ya Mbu.

     Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt Dorothy Gwajima amewata Wakurugenzi wa Halimashauri kuweka bajeti ya fedha kwa lengo la kununulia dawa kwa ajili ya kupulizia wadudu waenezao magonjwa mbalimbali kama malaria hususani Mbu kama mkakati mmojawapo wa kuhakikisha kuwa Tanzania inatokomeza ugonjwa huo nchini kutoka maambukizo ya asilimia 7.3 hivi sasa hadi asilimia 1 ifikapo mwaka 2030.
    Sambamba na hilo, Wakurugenzi wa halmashauri wametakiwa kulipa madeni yao baada ya kuchukua dawa za kupulizia wadudu katika kiwanda cha kutengeneza dawa hizo kilichopo kibaha, mkoani Pwani.















    Hayo amezungumza jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt Dorothy Gwajima mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wanaohusika katika kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini.
      Aidha,ameeleza kwamba hatarajii katika bajeti zijazo, kuona halmashauri hazitengi fedha kwa ajili ya kudhibiti na kutokomeza mazalia ya mbu katika halmashauri zao kwani hazitapia
   “Haitapita bajeti ya halmashauri kama haitaweka mikakati ya kudhibiti Malaria sambamba na maelekezo tuliyokuwa tukiyapeleka na mafunzo ambayo tumekuwa tukiyatoa,” amefafanua.
   Lakini pia,Dkt Gwajima ameongeza kuwa ni muhimu fedha hizo zitengwe ili zitumike katika kutokomeza mazalia ya mbu kwani wataalamu wa halmashauri wanajua ni maeneo gani ya halmashauri yenye mazalia mengi ya mbu wanaoambukiza ugonjwa wa malaria.
       “Kwa hiyo lazima ionekane pale ni kiasi gani cha dawa kitaagizwa kutoka katika kiwanda chetu cha kibaha kinachozalisha dawa zinazotumika kupulizia kwenye mazalia ili kudhibiti ongezeko la wadudu hawa,” amesema na kuongeza:
   “Wakurugenzi hawa walichukua hizi dawa kibaha hawajalipa, kwanza walipe deni, kisha wapange kwenye bajeti zao kuhakikisha kuwa kazi hiyo inafanyika.”
   Amesema kuna maeneo kwenye halmashauri ambayo yanajulikana kabisa ndiyo yenye mazalia ya mbu na kwamba dawa ikipulizwa kwenye maeneo hayo tatizo linakwenda chini.
     Akizungumzia zaidi kuhusu hali ya maambukizo ya ugonjwa wa malaria nchini Dkt Gwajima amesema jitihada zinazofanyika kutokomeza ugonjwa huo nchini zinafanikiwa kwani maambukizo ya malaria nchini yamepungua hadi asilimia 7.3 kutoka asilimia 14.8 mwaka 2015/16.
     Amesema kupungua kwa maambukizi ya malaria kumetokana na kuwepo kwa mikakati mbalimbali ya kinga pia uwepo wa dawa zinazotumika kupambana na ugonjwa huo ambapo kiwango cha matumizi yake kilifikia asilimia 98.4, huku matumizi ya kipimo cha haraka cha kupima vijidudu vya malaria (mRDTs) ikifikia asilimia 97.8, lakini pia kumekuwa na ongezeko la matumizi ya vyandarua vyenye dawa kwa asilimia 62.5 mwaka 2017 kulinganisha na asilimia 55.9 mwaka 2015/16.
     Kwa upande wake Meneja Mpango wa kudhibiti Malaria nchini Dkt Ali Mohamed amesema kulingana na takwimu za mwaka 2017, mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita, Mara,Lindi, Ruvuma na Mtwara inaonekana kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya malaria.
     Amesema kutokana na takwimu hizo, maeneo hayo yanayoonekana kuwa na kiasi kikubwa cha maambukizi ipo haja ya kupelekwa mikakati ya ziada mbali na mikakati ya kawaida ya kuzuia mbu, kuhakikisha kuna vitendanishi vya kupima malaria na dawa za kutosha zina ubora unaotakiwa.
     Ameitaja mikakati ya ziada ni jinsi ya kutumia dawa kinga (SP) kwa ajili ya wanafunzi shuleni, pia kutoa dawa katika maeneo ambayo malaria inapatikana kwa kipindi kichache, na mikakati mingine ambayo hufanywa na Mpango wa kudhibiti Malaria nchini.
    Juhudi za kuutokomeza ugonjwa wa malaria nchini, barani Afrika na duniani kwa ujumla bado una safari ndefu kwani kwa mujibu wa taarifa ya dunia ya malaria ya mwaka 2018 inaonyesha kuwa zimeripotiwa kesi milioni 219 za malaria duniani na kusababisha vifo 435,000.
   Hata hivyo,Barani Afrika katika asilimia 70 ya kesi zilizolipotiwa ni asilimia 71 ya idadi ya vifo  pia inatoka barani Afrika hasa katika nchi kumi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania. Nchi nyinginezo ni Burkina Faso, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ghana, Mali, Msumbiji, Niger, Nigeria na Uganda.
   Imeripotiwa na Mwandishi wetu;Adolf Mwingira.



   




No comments

Powered by Blogger.