Header Ads

Header ADS

Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga imewahukumu watu wa nne kifungo cha maisha Jela .

Watu wanne wamehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kutaka kumuua mtu mwenye ulemavu wa ngozi(Albino).

Mahakama Kuu kanda ya Sumbawanga imewatia hatiani watu hao kwa kumkata mkono wake Albino huyo kisha kuondoka nao kwa lengo la kwenda kuuza kwa Mganga wa jadi kwa gharama ya Tsh.Millioni 6 [sita]


Baada ya kuuchukua mkono huo(mzima), wamedai walienda kuubanika kwenye moto ili iwe rahisi kuusafirisha na kwenda kuuza kwa mganga wa jadi aliyewaagiza wamtafutie mkono wa Albino.

Mahakama hiyo imemuachia huru mshtakiwa wa sita Masunga Kashindye na baada ya kuachiwa alitimua mbio na kutokomea kusikojulikana, mshitakiwa wa tano Michael Samuel alifariki Dunia wakati akiwa Mahabusu.



No comments

Powered by Blogger.