Header Ads

Header ADS

Makonda Amtaka Mkandarasi Wa Jengo la Ghorofa Tano Kuongeza Kasi

 Paul Makonda  ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ametembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la ghorofa tano la mama na mtoto hospitali ya rufaa ya Mwananyamala na kumtaka mkandarasi wa jengo hilo Kutoka Chuo cha Sayansi na teknolojia Mbeya kuongeza kasi na masaa ya kazi ili akabidhi jengo hilo kabla ya Disemba 30 mwaka huu.
  Aidha Makonda amesema ujenzi wa Jengo hilo ulisimama tangu mwaka 2014 lakini kupitia uongozi thabiti wa Rais Dkt. John Magufuli aliona changamoto hiyo na kuamua kutoa zaidi ya Shilingi Billion 2.1 kwaajili ya kukamilisha ujenzi huo ili kupunguza kero kwa wananchi.












Hata hivyo amesema Jengo hilo litaanza kutumika mwezi January mwakani ambapo ndani yake litakuwa na uwezo wa kuchukuwa Vitanda 100 vya Mama na Mtoto na fedha ya kununua Vifaa tiba ipo tayari. Makonda Pia Amesema mbali na ujenzi wa Jengo hilo Serikali inaendelea na ujenzi wa Hospital ya wilaya Mabwepande na tayari yupo kwenye hatua za kujenga Kituo cha Afya Kawe na Bunju ambapo miradi yote ikikamilika itasaidia kumaliza Changamoto za Afya Wilaya ya Kinondoni.
   

No comments

Powered by Blogger.