Header Ads

Header ADS

Mchungaji aswekwa rumande Mkoani Njombe

           Watu wawili akiwemo mchungaji wa kanisa la Baptist Milton Mkunge lililopo  kijiji cha Mawindi wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe wamesomewa mashtaka matatu ya kujeruhi kinyume na sheria.
Akiwasomea mashtaka hayo,mwendesha mashtaka wa serikali wakili Happiness Makungu,amesema mshatikiwa wa kwanza Milton Mkunge (56),Mbena na mkazi wa kijiji cha Mawindi,hukuMshatikwa wa pili ni Nolbat Mkude mbena (45),Mkristu na mkazi wa kijiji cha Muhaji wote wanashtakiwa na makosa matatu ya kujeruhi kinyume na kifungu cha 225 cha  sheria ya kanuni ya adhabu sura namba 16 marejeo ya mwaka 2002    
Wakili Happiness amesema kosa la kwanza,la pili na la tatu mnamo tarehe 13-10-2019 huko katika kijiji cha Mawindi washtakiwa hao walimjeruhi Elesia fwimi,Rejina Lyahumi pamoja na Shaibu Mhema huko katika kijiji cha Mawindi.

Aidha washtakiwa hao wamekana mashtaka hayo na kurudishwa Lumande huku dhamana yao ikiwa wazi mpaka watakapoweza kukidhi vigezo vya dhamana zao ikiwemo wadhamini watatu,barua kutoka kwa watendaji wa kata,vitambulisho vyao pamoja na bondi ya shilingi milioni tatu.

Hata hivyo wakili wa mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Njombe Irvan Msack  ameahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 31 mwezi wa 10 mwaka 2019 ushahidi utakapokamilika na kusomwa tena.

Ikumbukwe kuwa siku kadhaa zilizopita  baadhi ya waumini wa kanisa hilo  kwa nyakati tofauti wakati wakihojiwa na vyombo vya habari waliwatupia lawama viongozi wao kwa kuwacharaza bakora kwa madai ni njia ya kutubu dhambi zao.

No comments

Powered by Blogger.