Header Ads

Header ADS

Mizengo Pinda apewa Sifa na Rais Magufuli

Rais wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Amempongeza Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda na Kuongeza Kuwa anamsaidia sana.
  “Leo ilitakiwa awepo hapa Mzee Pinda ananisaidia sana katika kazi, yule baba ana moyo wa kipekee,” Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo mkoani Katavi wakati wa uzinduzi wa barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni.
  “Ni mtu mwema sana  na ndio maana nimemchagua kuwa  mjumbe wa  kamati kuu. Ananisaidia kuongoza nchi, chama katika mambo mbalimbali kwa sababu ni mtu mmoja mstaarabu sana,”















Aidha ameendelea kusema kuwa  “Na ndio maana nimemtuma China akaniwakilishe katika maadhimisho ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere. Niliona  sina mwingine wa kumtuma atakayeniwakilisha vizuri nikasema Mizengo Pinda ndio aende, ni baba mwenye moyo wa tofauti.”

No comments

Powered by Blogger.