Header Ads

Header ADS

Mkuu Wa Majeshi Ya Ulinzi Na CDF Ameongoza Kamati Ya Ulinzi Na Usalama Kukagua Mpaka Wa Tanzania Na Msumbiji

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na CDF, Generali Venance MabeyoAmeongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Taifa na Kukagua mpaka wa Tanzania na Msumbiji. 











Hata hivyo Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wametembelea mpaka wa Tanzania na Msumbiji kwa lengo la kuhakikisha mpaka huo na wananchi wa maeneo hayo wako salama, hatua hiyo imekuja baada ya kusemekana nchini Msumbiji kunavitendo vinavyoashilia Ugaidi vinaendelea nchini humo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini CDF, General Venance Salvatory Mabeyo, huku akisisitiza kuwa kwa sasa mpaka uko salama na wakazi wa maeneo hayo wanatakiwa kuendelea na majukumu yao ya kila siku pasipo kuwa na wasiwasi.
Pia, kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema hali ya nchi kwa sasa ni salama na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kuendelea kudumisha amani na usalama nchini kwetu.

No comments

Powered by Blogger.