Header Ads

Header ADS

Mtuhumiwa wa Uhujumu Uchumi Vitambulisho Vya Taifa akiri kosa.

Astery Ndege ambaye ni mmoja  kati ya watuhumiwa wa uhujumu uchumi wa Vitambulisho vya Taifa amehukumiwa kulipa fidia ya gharama ya sh.293,446,400.23 kama hasara aliyosababisha kwa mamlaka hiyo kufuatia kukiri kosa.
   Ndege ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers ameachiwa huru peke yake huku watuhumiwa wengine ambao ni Mkurugenzi wa NIDA Dickson Maimu,Meneja wa Biashara NIDA Avelin Mamburi,Ofisa Usafirishaji George Ntalima,Mkurugenzi wa Sheria Sabisa Raymond na Xavery Kayombo wakiendelea kusalia rumande.













Hata hivyo hatua hiyo imefuatia baada ya Ndege kuandika barua ya kukiri kosa na kuomba msamaha kwa DPP baada ya kuisababishia NIDA hasara zaidi ya bilioni 1.1
  Wakati akisoma hukumu hiyo,hakimu mkazi mwandamizi  Salum Ally amesema mshitakiwa atatakiwa kulipa milion nne kama faini ya kuongoza genge la wahalifu iliyopelekea kuingizia NIDA hasara hiyo.
   Pia,wakili wa Serikali Mwandamizi Ladislaus Komanya aliwasomea watuhumiwa wote mashtaka 50 badala ya mashtaka 100 waliyokuwa wakikabiliana nayo awali ambapo amedai wanakabiliwa na mashtaka hamsini yakiwemo ya kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri,kughushi,kutoa nyaraka za uongo,kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya sh.1,175,785,600.93 kwa NIDA.
   Hata hivyo Ndege ndiye pekee aliyekiri kosa hilo la kujihusisha na genge la uhalifu na kusababisha hasara ya bilion moja huku wenzake wakikana makosa hayo.
   Kufuatia kukiri mwenyewe, mahakama ilimtia hatiani.

Wakili Komanya aliiomba mahakama kutoa adhabu kwa mshitakiwa kulingana na makubaliano waliyoingia. Pia amedai mshitakiwa ni mkosaji wa mara ya kwanza na kwamba kitendo cha kaomba msamaha kitasaidia kupunguza msongamano wa watu gerezani. 

Kwa upande wake wakili wa utetezi, Godwin Nyaisa amedai mshitakiwa hajaisumbua mahakama kwa kuwa amekiri na anajutia kosa lake na tayari amekubali kurejesha sehemu ya hasara kama ilivyoainishwa kwenye makubaliano yao.

Amedai mpaka sasa mshitakiwa amekaa gerezani miezi 10 hivyo, anaomba apatiwe adhabu ya faini.

No comments

Powered by Blogger.