Header Ads

Header ADS

Mvua Kubwa Yaleta Maafa Morogoro

 Wanafunzi watano wa Shule ya Msingi Nyachilo, wameripotiwa kufariki dunia kufuatia mvua kubwa, zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Morogoro.Na kupelekea kuwa na Jumla ya Watu tisa waliofariki.
  Wilbroad Mtafungwa ambaye ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, amesema watu hao wamekufa maji katika matukio tofauti na sehemu tofauti, ikiwemo wanafunzi watano kusombwa na maji katika Mto Mvuha, wakati wakitoka shuleni.











Aidha watu wengine wawili wakielezwa kupotea baada ya kuzama kwenye Bwawa la kuhifadhia maji machafu ya  linalomilikiwa na kiwanda cha Sukari cha Kilombero.
   Kamanda Mutafungwa amewataja waliokufa katika matukio hayo kuwa ni Rajabu Issa, Shabani Msimbe,Neema Rajabu,  Latifa  Khalidi, Munira Khalid, Omary Khalidi ambao miili yao imepatikana huku mmoja wao Zainabu  Rajabu, mwili wake bado haujapatikana mpaka hivi sasa.
 Pia, ametoa wito kwa wananchi, wazazi na walimu kuhakikisha wanakaa karibu na Watoto wao ili kuhakikisha wanakuwa salama kipindi hiki cha mvua ili kuepusha maafa yanazidi jitokeza.
  NA MWANDISHI DIANA MALEKELA,MOROGORO
    
  

No comments

Powered by Blogger.