Header Ads

Header ADS

Prof.Kitila Asisitiza Watendaji Sekta Ya Maji Kutofanya Kazi Kwa Mazoea

  Katibu Mkuu Wizara ya Maji,  Profesa Kitila Mkumbo amewataka watendaji  wa mamlaka za maji nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawe wabunifu ili kukuza mapato ya sekta hiyo.Aliyasema hayo  alipokutana na wakurugenzi wa mamlaka za maji na watendaji wakuu wa sekta hiyo wakati akifungua mkutano wa uendeshaji wa kisekta mjini Singida leo.

” Zamani mamlaka za maji zilikuwa zikitoa huduma lakini sasa hivi zinaendelea kutoa huduma na pia ujenzi wa miradi ya maji haya ni mabadiliko makubwa sana kisekta hivyo zingatieni ubunifu katika utendaji wenu” alisema Mkumbo.

 Aidha Kitila Alisema kutokana na mabadiliko hayo kuna kila sababu ya kupitia muundo mpya wa utumishi kuanzia ngazi ya wizara na taasisi ili kuiweka katika mifumo inayoeleweka.

 Aliongeza Pia, kupitia mfumo huo mpya itasaidia taasisi husika kuweza kuchagua wahandisi wenye viwango stahiki kukidhi matarajio ya miradi kwa ufanisi.

“Tunakusudia kuanza kuzingatia vigezo ikiwemo kuangalia ni mradi gani apewe mkandarasi kulingana na sifa na uwezo alionao kuweza kusimamia mradi husika” alisema.

Hata hivyo,Mkumbo alisisitiza kuwa yote hayo yatawezekana kama kutakuwepo na ushirikiano wa dhati baina wa watendaji wa sekta ya maji na wadau wote kwa ujumla.

No comments

Powered by Blogger.