Header Ads

Header ADS

SADC Yatakiwa Kuweka Mikakati Ya Pamoja Ya Kukabiliana Na Viumbe Vamizi

 Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezitaka nchi za SADC kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na viumbe vamizi ambao ni changamoto kubwa katika nchi wanachama kwani wamekua na athari kubwa katika mazingira na uchumi.


 Aidha Akizungumza wakati akifungua mkutano wa Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii wa Nchi za SADC amesema kuwa suala la viumbe vamizi ni tishio kubwa kwa mazingira kwani linathari kubwa.

“Jumuiya iangalie uwezekano wa kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na viumbe vamizi na pia mikakati hiyo itekelezwe,” Alisema Samia.

Pia, amewata Mawaziri wa jumuiya hiyo na wataalamu kushirikiana katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo zimekua na athari kubwa ikiwemo mafuriko, ongezeko la magonjwa ya mlipuko na Ukame.

Makamu wa Rais amesema kuwa nchi za Afrika zimebarikiwa kuwa na vivutio vya utalii ambavyo vimekua vikichangia Dola milioni 56.3 sawa na asilimia 8% ya fedha ya pato ghafi na takriban ajira milioni 6 kwa watu walioko katika ukanda wa SADC.

Hata hivyo,Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla amesema kuwa nchi za SADC zina itifaki ya pamoja ya kukuza na kuendeleza utalii hivyo zikitumia fursa za vivutio hivyo zinaweza kupiga hatua na sekta ya utalii ikachangia mapato makubwa.

No comments

Powered by Blogger.