Header Ads

Header ADS

Silaha Mbili Aina Ya Short Gun Zakamatwa Mbeya Kufuatia Msako Mkali

  Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limekamata silaha mbili aina ya Short Gun zikiwa na risasi mbili ambazo zilikuwa kwenye mtutu wa kila silaha ambazo zilikuwa zimefichwa kwenye mfuko wa plastiki.

















  Hata hivyo,Kufuatia msako mkali uliofanyika Oktoba 17, 2019 saa 17:00 jioni huko maeneo ya Pambogo, mtaa wa Isengo, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jiji la Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilikamata silaha hizo ambazo zimetengenezwa kienyeji na baada ya kuzikagua zilibainika kutokuwa na namba za usajili zozote.
 Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ametoa  rai kwa wananchi kutoa taarifa za mtu/watu au kikundi cha watu ambacho wanakitilia mashaka katika maeneo yao ili ufuatiliaji ufanyike haraka iwezekanavyo.
   Pia, ametoa taarifa kwa mtu yeyote anayemiliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha silaha hiyo mara moja kituo cha Polisi kabla Jeshi la polisi kuanza kufanya upekuzi.

No comments

Powered by Blogger.