TAKUKURU Mkoani Kagera Yamshikilia Kaimu MenejaMkuu Wa Kampuni Ya Ranchi Za Taifa(NARCO)
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Kagera inamshikilia kaimu Meneja mkuu wa kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) Profesa Philemon Nyangi Wambura kwa tuhuma ya matumizi mabaya ya ofisi,kuomba na kupokea rushwa kiasi cha shilingi million 12.
Aidha,Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera Bw.John Joseph amesema septemba 23 mwaka huu taasisi hiyo ilipata taarifa ambayo ilionyesha kuwa mtuhumiwa aliomba na kupokea rushwa kiasi cha shilingi million 12 kutoka kwa mtu mmoja kwa lengo la kumpatia kitalu kwa ajili ya kufanyia shughuli za ufugaji.
Joseph amesema kuwa wakati upelelezi ukiendelea wanatarajia kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo ili aweze kujibu mashitaka yanayomkabili.
“Taarifa ya uchunguzi inaonesha kwamba Tarehe 03/01/2018 Prof.Philemon Nyangi Wambura akiwa kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), alipokea jumla ya shilingi milioni kumi na mbili (12,000,000/=) kutoka kwa mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa ili aweze kumpatia kitalu kwaajili ya kufanyia shughuli za ufugaji huku akifahamu kuwa jambo hilo ni kosa na kinyume cha sheri na sasa mnamo tarehe 23/09/2019 tulimkamata na tutampeleka mahakamani.” Amesema Kamanda Joseph.
Aidha Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Kagera pia imewafikisha mahakamani watu wanne kwa makosa tofauti yakiwemo ya kugushi nyaraka kwa ajili ya kujipatia fedha kinyume cha sheria.
Hata hivyo,Kamanda Joseph amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Stanslous Katto mwenyekiti wa kamati ya sekondari kashenye,bw,Richard Mchumi mwenyekiti wa kijiji cha mkalinzi wilayani Ngara, Josephat Ndezekahino ambaye pia ni mtendaji wa kijiji cha mkalinzi na Onesimo Mbadiliko Tiara mwenyekiti wa kamati ya vocha za pembenjeo wa kata ya Muganza wilayani Ngara
Mkuu huyo wa takukuru amewasihi wananchi mkoani Kagera kuendelea kutoa ushirikiano na taasisi hiyo na taarifa za kuwabaini wala rushwa na mafisadi wanaotumia vibaya madaraka waliyopewa na serikali.
No comments
Post a Comment