Header Ads

Header ADS

Wakazi wa kagera washauriwa kujenga majengo Imara.

Wakazi Mkoani kagera Washauriwa kujenga majengo imara kwakufuata taratibu zote ili kuepuka maafa yanayojitokeza.
  Hayo yamesemwa leo Oktoba 13,2019.Na Mwenyekiti wa kamati ya Maafa Mkoani Kagera ambaye Pia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Kagera Prf, Faustin Kamuzora wakati  akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake ikiwa leo ni siku ya kitaifa ya kupunguza Maafa Duniani.
   
  "Sisi kama mkoa tunatumia siku hii kuwataka wananchi kujiepusha na maafa mbali mbali na pia Halmashauri ziboreshe sheria ya majengo imara ili kujikinga na madhara", alisema Kamuzora.
  Amesema wananchi kabla ya kujenga watafute sehemu sahihi kwa kujiepusha kujenga sehemu za mabondeni,
   Pia, Profesa Kamuzora ameeleza kuwa kutokana na madhara makubwa ambayo yamekuwa  yakiukumba mkoa wa  Kagera  ikiwemo tukio la Septemba 2016 la tetemeko la Ardhi lenye mkubwa 5.9 katika vipimo vya Richter na mengine mengi wananchi wanapaswa kutumia siku hii kujenga majengo yaliyo imara kwa kufuata taratibu zote za ujenzi ili kuepuka na maafa ambayo yamekuwa yakijitokeza nakuleta athari kubwa.
   Hata ivyo, amesema mkoa wa Kagera umechukua hatua endelevu kupunguza uharibifu wa maafa katika miundo mbinu na kuendelea kuelimisha wananchi kujenga majengo imara na kufuata taratibu za ujenzi.
  pia,amezitaka Halmashauri za mkoa huo kusafisha mifereji kila wakati ili kuruhusu Maji kupita na kutiririka na kuelekea katika sehemu husika ili kuepuka mafuriko yanayoweza kuleta maafa na madhara makubwa katika mkoa huo.
Hata hivyo amesema mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watahakikisha wanatoa elimu zaidi kwa wananchi ili waweze kupambana na maafa.

No comments

Powered by Blogger.