Wanachuo Wavalishwa Maboksi Kuondoa Udanganyifu Wakati Wa Mtihani
Mamlaka ya usimamizi wa shule nchini India umewataka Chuo cha The Bhagat kandika barua ya maelezo na kuomba msamaha kufuatia tukio lao la majaribio walilolifanya kwa wanafunzi kuwavalisha mabox kichwani kwa lengo la kutaka kukomesha tabia ya wanafunzi kupigiana chabo wakati wa kufanya mitihani yao.Taarifa za chuo hicho kufanya tukio hilo, zilisambaa baada ya kupostiwa katika mtandao wa kijamii wa Facebook na mmoja wa wafanyakazi katika chuo hicho cha The Bhagat.
“Hakuna mwanafunzi aliyelazimishwa kuvalia boksi kichwani. Kama unavyoona katika picha hizi kuna baadhi ya wanafunzi ambao hawajayaavaa, waliokuwa wameyavaa waliyavua baada ya dakika 15, wengine baada ya dakika 20 na hata sisi wenyewe tuliwaambia wayavue baada ya saa moja,” amesema MB Satish.
Kwa mujibu Wa Maelezo yao wameeleza kuwa kati ya wanafunzi 72 ni wanafunzi 56 tu ndio walikubali kuvaa maboxi kama sehemu ya jaribio hilo.wanajisikia vizuri na jaribio hilo na chuo hakijamsumbua mwanafunzi yeyote kuhusu suala la kuvaa maboksi hayo,” amesema MB Satish.
No comments
Post a Comment