Header Ads

Header ADS

Wanafunzi 8 watiwa Mbaroni kwa Tuhuma za kumuua mwanafunzi mwenzao Kahama.

Jeshi la Polisi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga linawashikilia wanafunzi nane wa shule ya Sekondari Seeke kwa tuhuma za kumuua  za kumuua na kumshambulia mwanafunzi mwenzao Constatine Makoye mwanafunzi mwenzao majeraha ambayo yamesababisha kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Halmashauri ya Mji Kahama.














ACP Richard Abwao ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga amethibitisha suala hilo la kushikiliwa kwa wanafunzi hao wanaotuhumiwa kufanya mauaji hao ambalo limetokea Septemba 2019 katika kanisa la SDA Wasabato Kahama ambapo kulikuwa na Sherehe ya kuwaaga wanafunzi washirika  wa kanisa hilo wanaotarajia kuhitimu kidato cha nne.
   Aidha Kamanda Abwao ameorodhesha majina ya wanafunzi hao wanaotuhumiwa ambao ni:
1. Isaya  Athuman 18, Muha, mkazi wa nyahanga.

2. Godfrey Fanuel Simon, 18, Mnyiramba, mkazi wa shunu

3.Enock Lazaro Alfred, 17, Mhangaza, Mkazi wa Shunu.

4. Athuman Azizi, 17, Mnyamwezi, mkazi wa shunu,

5. Leonard Emmanuel Lutonja, 17, Msukuma, mkazi wa shunu.

6. Michael Philipo 17, msukuma, Mkazi wa Shunu.

7 . Sadiki Boniface stephen, 18, mfipa, mkazi wa legela
8 .emmanuel musa Sekela, 18, Muha, mkazi wa shunu
Pia ameeleza kuwa baada ya Sherehe kuisha katika kanisa hilo alitokea mwanafunzi huyo ambaye ni Constatine Makoye akiwa na vijana wenzie kumi ambao hawakufahamika kwa haraka kama walikuwa ni miongoni mwa waalikwa katika Sherehe hiyo.
  Wanafunzi hao walimkamata Isaya Athuman(18) mwanafunzi wa kidato cha nne na kutaka kumnyang'anya viatu alivyokuwa amevaa na kunyang'anya maji ya kunywa kwa wanafunzi waliokuwepo kwenye sherehe hiyo.
   Ndipo wanafunzi hao walipiga kelele ili kutaka kusaidiwa na kuanza kuwarushia mawe wavamizi hao lakini wavamizi hao walikimbia na kutawanyika lakini Constatine Makoye alionekana kuzidiwa na kulala chini na wanafunzi hao walimtelekeza hapohapo akihangaika.
  Constatine aliamka na kuenda kumueleza babu yake ambaye alimpeleka kutibiwa katika hospitali ya Wilayani Kahama bila kutoa taarifa kituoni mpaka alipozidiwa 01/10/2019 na ndipo ndugu walipofungua jarada kwa kosa la kujeruhi lakini maelezo ya mwanafunzi huyo hayakutolewa kutokana na hali yake kuwa mbaya.
    Mnamo Tarehe 02/10/2019 mwanafunzi huyo alifariki dunia na mwili wake ulipimwa na kuonekana kuwa chanzo ni Madhara makubwa aliyoyapata kichwani na mwili huo umeshakabidhiwa kwa ndugu zake.Lakini chanzo cha kifo kimeelezwa kuwa ni Ugomvi uliokuwepo baina ya marehemu na watuhumiwa kwa madai ya kuwa ni mwizi.

   
 

No comments

Powered by Blogger.