Wazazi wanaowakatisha wanafunzi masomo Mkoani Iringa Waonywa.
katika mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Mlafu iliyopo katika kijiji cha Mlafu wilayani Kilolo Mjumbe wa halmashauri Kuu (CCM) Mkoa wa Iringa, Leah Mwamoto amewaonya wazazi wanaokatisha masomo watoto kuwa serikali itawachukulia hatua kali pindi watakapobainika kufanya kosa hilo,ambapo alimwakilisha mbunge wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto.
Akiwaonya wazazi katika mahafali hayo Mwamoto amewaeleza wazazi juu ya mazingira mabaya wanayoyakuta watoto wanaokwenda kufanya kazi za ndani katika miji mikubwa.
Lakini pia,amewataka watendaji wa kata kuendelea kuwafutilia watoto ili kuwaepusha kujiingiza katika mazingira hatarishi yatakayoharibu ndoto zao.
Hali kadharika Mwamoto ametoa pongezi kwa uongozi wa shule ya sekondari Mlafu kwa matokeo mazuri pamoja na mbunge wa jimbo la Kilolo, Mhe Venance Mwamoto kuchangia bati 180 na mifuko 100 ya saruji kwa ujenzi wa zahanati kijiji cha Mlafu.
Aidha,awali Mkuu wa shule Emmanuel Mbangwa wakati akisoma taarifa fupi ameomba wadau kujitokeza kuboresha mazingira katika shule hiyo hususani kujenga nyumba za walimu na mabweni.
Kwa upande wake Diwani Mlafu Isidory Kiyenge amewaomba wadau wa kata hiyo pamoja na wazazi kuwa tayari kuchangia katika sekta ya elimu ili kuongeza mazingira ya ufaulu.
Aidha,Kayenge ametoa ahadi ya kuwaandalia wanafunzi wa kidato cha nne chakula wakati wa mitihani yao sambamba na hilo amewataka wanafunzi wa shule hiyo kujiandaa vyema na mitahani yao inayowakabili.
Imeripotiwa na Mwandishi wetu;Adolf Mwingira.
No comments
Post a Comment