Header Ads

Header ADS

Waziri Wa Nishati Dkt.Medard Kalemani Atoa Maagizo Kwa Viongozi 11

   Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amewata viongozi wa mikoa 11 inayoguswa moja kwa moja na upatikanaji wa maji mto Rufuji kwa ajili ya utosherevu wa katika uzalishaji wa umeme wa maporomoko ya maji ya mto Rufiji wa Julius Nyerere, kuhakikisha wanahamasisha wananchi kulinda na kutunza vyanzo vyake vya maji na kutumia maji yaliyopo vizuri kwa shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi ili mradi huo ukikamilika uweze kujiendesha wenyewe.

 Waziri Kalemani alisema hayo jana baada ya kutembelea mradi huo mkubwa wa kuzalisha umeme kwa Megawati 2,115 akiwambatana na Naibu Waziri wa anayesimamia shughuli zote za ujenzi nchini Misri , Mhandisi Mahmoud Nssar ,na hiyo ikiwa ni mara yake ya tisa kufanya hivyo kwa lengo la kujionea maendeleo ya kazi zinazofanywa na mkandarasi, kubaini changamoto za kiusimamizi na manufaa na fursa hasa kipindi cha utekelezaji.

Aidha,Dk Kalemani alisema licha ya kuridhishwa na kasi ya ujenzi kuendana na muda, na kuahidi kila mwezi kufika kuukagua Ujenzi huo.

Pia alimwagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo kupitia kamati iliyoundwa kukutana na viongozi wa mikoa 11 inayoguswa moja kwa moja na upatikanaji wa maji , lazima viongozi wake wakutane na kuhamasisha wananchi kuanzia ngazi ya vijiji, kata na tarafa ili ulindwaji na utunzwaji wa vyanzo uwe ni endelevu.

Waziri pia alitembelea ujenzi wa nyumba za kudumu za wakandarasi na wasimamizi zitakazokamilika Desemba mwaka huu, maeneo ya kupitisha maji, ujenzi wa mashine tisa ulioanza wiki tatu kabla ya muda wake na eneo la krasha la kusaga simenti na konkriti.

Aidha, waziri Kalemani akawakumbusha wakandarasi kuzingatia ajira asilimia 80 kwa watanzania isipokuwa kwa kazi za ulinzi,usafi, upishi,zifanywe kwa asilimia 100 sambamba na ununuzi wa malighafi za ujenzi,vyakula na maji.

 Hata hivyo,Mradi huu unapata maji kutoka kwenye mito mikuu mitatu ambayo ni Mto Ruaha Mkuu unaochangia asilimia 15 ya maji, Mto Kilombero unaochangia asilimia 65 ya maji na Mto Luwegu unaochangia asilimia 19 ya maji. Waziri pia alitoa miezi miwili kwa barabara ya lami ya kilometa 60 kutoka Fuga hadi eneo la mradi ianze Kutengenezwa.

No comments

Powered by Blogger.