Zaidi Ya Wanafunzi 350 Wamekatisha Masomo Kutokana Na Utoro Na Mimba
Wanafunzi 350 Kati ya 602 waliotakiwa kuhudhuria masomo katika shule ya sekondari Marumba Halmashauri ya wilaya Tunduru wamekatisha masomo yao kutokana na utoro na Mimba.
Mkuu wa Shule hiyo Michael Kapinga amesema hayo wakati wa mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo na kuongeza kuwa wanafunzi hao waliokatisha masomo ni wale waliochaguliwa kuanza masomo ya Sekondari katika kipindi Cha miaka minne kutoka mwaka 2016 hadi mwaka 2019.
Hata hivyo,Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Chama Cha Walimu Taifa Sabina Lipukila ameagiza kusakwa wanafunzi wote waliotoroka na kukatisha masomo yao ili warudi Shule na kuendelea na masomo.
Aidha amewataka watendaji wa vijiji na kata kuwakamata wazazi wa wanafunzi hao na kufikishwa mahamani na kuhojiwa.

No comments
Post a Comment