Abiria wanusurika kuungua moto
Abiria ambao idadi yao haijajulikana wamenusurika kuungua baada ya gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T998 AAP linalofanya safari zake Shinyanga kwenda Maswa kuteketea kwa moto.
Tukio hilo limetokeo leo Ijumaa Novemba 29,2019 majira ya saa nane na nusu wakati abiria wakiwa wamepanda kwenye Hiace hiyo wakijiandaa kuanza safari kuelekea Maswa mkoani Simiyu.
Dereva wa Hiace hiyo aliyejulikana kwa jina Basu Gereja amesema chanzo ni kupasuka kwa Betri na kusababisha gari hilo kuwaka moto.
"Chanzo ni Betri kulipuka,tumefanya utaratibu wa kuwatoa abiria kwenye gari kisha kupiga simu Zimamoto kwa ajili ya msaada ambao wamefika na kusaidia kuzima moto huu,gari ilikuwa inatoka Shinyanga kwenda Maswa",amesema Basu.
Kutokana na mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Machweo Communication News kuwa dereva alikuwa amewasha gari akijiandaa na safari ndipo ghafla walipoona gari linawaka moto ndipo utaratibu wa kuwatoa abiria ukaanza kufanyika huku abiria wengine wakitokea madirishani kwa sababu mlango uligoma kufunguka.
Mratibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga Edward Lukuba (Afisa Oparesheni Mkoa wa Shinyanga) amesema wamepata taarifa za kuteketea gari kwa kuchelewa na kukuta gari hilo linaungua na kufanikiwa kuzima moto huo huku akiwasisitiza wananchi kujitahidi kuwa wanatoa taarifa mapema pindi majanga yanapotokea.
No comments
Post a Comment