Bondia Hassan Mwakinyo amchapa Mfilipino Tinampay bila huruma
Bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo amefanikiwa kushinda pambano lake dhidi ya Arnel Tinampay.
Pambano hilo lilikuwa la raundi 10 na kufanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na Mwakinyo ameibuka na ushindi wa pointi.
Kwenye pambano hilo jaji wa kwanza alitoa alama 97-93, jaji wa pili 98-92, na jaji wa tatu alitoa alama 96-96.
Hilo lilikuwa ni pambano la 18 kwa Mwakinyo ambapo ameweza kushinda mapambano 16 na kupigwa mawili.
No comments
Post a Comment