Header Ads

Header ADS

Dkt, Mabula awatuliza wananchi Wanaodai Fidia ya maeneo yao Dodoma.

Naibu Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewatuliza takribani wananchi 49 wa eneo la Mtumba, Dodoma waliokuwa na hasira ya madai ya kutolipwa fidia maeneo yao ulipojengwa Mji wa Serikali.
Dkt Mabula aliwatuliza wananchi hao leo tarehe 11 Novemba 2019 jijini Dodona walipoandamana kuelekea ofisi za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi jijini Dodoma baada ya jitihada zao za kupatiwa fidia ya maeneo yao kushindwa kupatiwa ufumbuzi na ofisi ya jiji la Dodoma.

Pia,Dkt Mabula alisema, Wizara yake imeyapokea malalamiko ya wananchi hao na kuwataka kuwa na subira hadi hapo uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakapomalizika tarehe 24 Novemba 2019 na kupata viongozi watakaoshirikiana nao wakati wa zoezi la uhakiki wa mipaka na kubaini wamiliki halali wa maeneo hayo.
Aidha,Kwa mujibu wa Dkt Mabula, Wizara yake haina uhakika na wamiliki wa maeneo hayo hadi hapo timu maalum itakapoenda kufanya uhakiki ambao kila mwananchi anayedai kuwa na eneo Mtumba athibitishwe sambamba na kujiridhisha kuwa maeneo hayo ni ya kwao kwa kuwa taarifa zinzonesha eneo wanalodai linamilikiwa na Jeshi.
‘’Suala la msingi hapa ni kutambua maeneo, maendelelezo yoyote katika eneo hilo yasiwatishe na cha msingi hapa ni kwenda uwandani kujiridhisha uhalali wa wamiliki’’ alisema Dkt Mabula.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi hao wameeleza kusikitishwa na jinsi wanavyozungushwa kupatiwa fidia za maeneo yao tangu mwaka 2016 jambo lililowafanya kuandamana hadi ofisi za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa lengo la kuonana na Waziri mwenye dhamana ya ardhi.
Pia,Mmoja kati ya wananchi hao Jakson Simon alisema, anashangazwa na jinsi wanavyohangaika na fidia kwa muda mrefu wakati uhakiki ulishafanywa mara kadhaa na jeshi kwa ushirikiano na maofisa wa Jiji la Dodoma lakini linapokuja suala la kulipwa fidia hakuna utekelezaji wowote.
Aidha,mwananchi Mwingine Geofrey Stephano alisema, maelezo kuwa eneo walilokuwa wakilimilki ni la jeshi hawakubaliani nalo kwa kuwa wao hawana ugomvi na Jeshi kwa kuwa uhakiki wa awali ulifanywa na jeshi hilo na kuanisha mipaka kati ya maeneo yao na jeshi.
Hata hivyo,Kwa muda sasa baadhi ya wananchi wanaodai kumiliki maeneo ulipo Mji wa Serikali Mtumba wamekuwa wakidai fidia na wengine wakidai kiasi walicholipwa kama fidia ni kidogo jambo lililosababisha kuhangaika ofisi mbalimbali kudai haki yao na sasa kuamua kuandamana hadi ofisi za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dodoma kuonana na Waziri wa Ardhi.


No comments

Powered by Blogger.