Dkt,Magufuli ameeleza mitazamo yake mitatu Juu ya Shahada aliyoipata.
Baada ya Rais Dkt. Joh Magufuli kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ameeleza jinsi alivyoipokea kwa furaha na kutoa mitazamo yake juu ya shahada hiyo.
Mtazamo wake wa kwanza ulianza kabla hajakubali wito wa kutunukiwa shahada hiyo ambapo ilimlazimu kujiuliza maswali mbalimbali na mwisho akapata jibu.
“Baada ya kuambiwa kwamba nitatunukiwa shahada ya udaktari wa falsafa nilijiuliza maswali mengi, lakini nilikubali baada ya kukumbuka kuwa mara nyingi shahada hizi za heshima hazitolewi kwa maana ya kumpa mtu binafsi bali zinakuwa kwa niaba ya watu wengine,” amesema Magufuli.
Hata hivyo,Dkt,Magufuli amesema kuwa anatambua kuwa shahada hiyo siyo yake binafsi bali ni ya watanzania wote, na huo ndiyo mtazamo wake wa pili juu ya shahada hiyo.
“Wakati napokea shahada hii ya heshima, kwa heshima, furaha, na unyeyekevu mkubwa, natambua kuwa si yangu binafsi bali ni ya Watanzania wote,” Ameeleza.
Pia, mtazamo wake wa tatu ni matokeo ya uongozi wake; mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano.
“shahada hii kimsingi imetolewa kutokana na mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya tano, mafanikio hayo hayatokani na juhudi zangu binafsi bali kwa ushirikiano wa watanzania wote.” Amesema Magufuli.
Hata hivyo ,Ikumbukwe ya kuwa Rais Magufuli ni kiongozi wa tatu kutunukiwa shahada ya heshima baada ya Rais mstaafu, Jakaya kikwete na Waziri mkuu msataafu, Rashidi Kawawa,kutoka katika chuo cha UDOM.
No comments
Post a Comment