Fedha za Kikoba za yeyuka kwenye kibubu kwa njia ya kishirikina.
katika kikundi cha ujasiriamali cha Imani Mkoani Arusha katika hatamu ya kugawana fedha imeingia doa baada ya baadhi yao kuzimia ghafla ukumbini kutokana na taarifa ya upotevu wa zaidi ya milioni 39 zinazodaiwa kuyeyuka kwa njia ya kishirikina. Hela hizo zinadaiwa ziliyeyuka ndani ya sanduku la fedha nyumbani kwa mweka hazina wa kikundi hicho chenye wanachama 20.
Aidha,mmoja wa wanakikundi, Grece Magala amesema kikundi chao chenye miaka mitano tangu kuanzishwa hawajawahi kugawana faida yoyote hadi juzi walipokaa na kukubaliana kugawana faida iliyopo. Wanakikundi hao waliambiwa fedha zimeyeyuka ndani katika mazingira ya kutatanisha jambo lililozua gumzo kwa wanachama wanawake waliokuwa wameambatana na waume zao ili kupokea gawio kwa lengo la kufanya manunuzi na mahitaji mengine ya majumbani kwao. Hata hivyo,Katibu wa kikundi hicho, Deogratius Seif amesema wanaendelea na ufuatiliaji na watakutana na viongozi wa kikundi kujua tatizo na watatoa taarifa kamili kuhusu upotevu wa fedha hizo.
No comments
Post a Comment