Header Ads

Header ADS

Hukumu ya Rais wa zamani wa TFF na wenzake watatu inatarajiwa kusomwa Disemba 5,Mwaka huu.

     Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema itatoa hukumu dhidi ya Rais wa zamani wa TFF Jamal Malinzi na wenzake watatu December 05 mwaka huu.
   Malinzi, Mwesigwa, Mwanga na Flora wanakabiliwa mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha Dola za Kimarekani 173,335.

     Hukumu hiyo ilitarajiwa kusomwa hapo jana lakini Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, alieleza hukumu hiyo bado haijakamilika na kwamba itasomwa tarehe iliyopangwa.
  Kesi hiyo imesikilizwa na Hakimu Mkazi Maira Kasonde lakini kwa sasa amehamishwa kituo cha kazi
  Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kusikiliza hukumu na upande wa Jamhuri ulikuwa tayari.
  Aidha, Hakimu Shaidi alisema hukumu ya kesi hiyo itasomwa Desemba 5, mwaka huu na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu.

No comments

Powered by Blogger.