Jeshi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kukamata bunduki mbili za kivita pamoja na nyara za serikali
Jeshi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kukamata bunduki mbili za
kivita pamoja na nyara za serikali ambazo ni nyama ya twiga pamoja na
vipande viwili vya meno ya tembo sambamba na silaha za jadi yakiwemo
mapanga,sime na visu.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa,Jonathan Shana alizitaja silaha
hizo kuwa ni AK 47 yenye namba 174364 ikiwa na risasi 6 kwenye
magazine na G3 yenye namba A36011858 ikiwa na risasi 9ndani ya
magazine na kwamba zilikamatwa katika eneo la Naani lililopo katika
mpaka wa Tanzania na Kenya tarafa ya Loliondo Mkoani hapa.
Aidha,alisema kuwa kukamatwa kwa silaha hizo kunatokana na ushirikiano kati ya
jeshi la polisi,Tanapa,Hifadhi ya Ngorongoro,kikosi dhidio ya
ujangili(KDU)Kanda ya kaskazini na kikosi kazi cha taifa
kinachopambana na ujangili kanda ya ziwa katika operesheni
inayorndelea huko Loliondo.
“Bunduki hizo zilipatikana baada ya majibizano ya risasi baina ya
kikosi kazi hicho kabambe na majangili mara baada ya kuona
mashambulizi yamezidi majangili hao walitelekeza silaha hizo na
kukimbilia nchi jirani,hata hivyo kikosi kikosi hicho kilifanikiwa
kumjeruhi kwa risasi jangili mmoja ambaye pia alifanikiwa kukimbia
huku akivuja damu”alisema Shana.
Kamanda huyo wa polisi aliongeza kuwa mnamo tarehe 10 mwezi wa 11
mwaka huu katika eneo la Oleng’usa kijiji na kata ya oloipiri ndani ya
eneo la pori tengefu la Loliondo walifanikiwa kukamata watu wawili
wanaojihusisha na ujangili ambao ni Yamhanga Mwita(19)na Chacha
Marwa(20) wakazi wa Serengeti Mkoani Mara wakiwa wameuwa Twiga.
Alisema kuwa watuhumiwa hao walikutwa wakiwa wanaendelea kuanika nyama
hizo porini kwa ajili ya kusafirisha baada ya kuwa wamezikata vipande
vipande ambapo ndio waliokutwa na panga,sime mbili,kisu tochi pamoja
na nyaya za kutegea wanyama zikiwa katika mafungu saba.
Kuhusu meno ya tembo alisema kuwa tarehe 10 mwezi wa 11 mwaka huu
majira ya 17:40,maeneo ya mbuyuni wilayani Arumeru waliwakamata watu
watano wakiwa na meno hayo pamoja na pikipiki mbili aina za Kinglion
namba T917 BUA na Sunlag namba MC 819 ACD ambapo walitokea wilayani
Simanjiro mkoani Manyara walipokuwa wameyahifadhi na kwamba walikuja Mkoani hapa kwa ajili ya kuyauza.
Kadhalika Kamanda Shana alisema kuwa polisi inawashikilia Juma
Yahaya(33)na Amani Mbise(32) wanaojishughulisha na kusajili laini za
simu,wakazi wa jijini hapa kwa tuhuma za kutumia jina la Gavana wa
benki kuu ya Tanzania(BOT)Profesa Frorence Luoga katika mitandao ya
kijamii na kuwatapeli watu mbalimbali kwa kutumia jina hilo ambapo
baada ya upelelezi wamekiri kosa hilo.
“Baada ya kuwapekuwa watuhumiwa tuliwakuta na simu 6,mashine mbili ya kusajili kwa alama za vidole,laini mbalimbali,vitambulisho 9 ya wateja
ambao walishawasajilia laini zao za simu na kwamba tumebabaini
mtuhumiwa huyu anamiliki jumba la kifahari eneo la Sombetini jijini
hapa hali ambayo aiendani na kipato chake”alisema
Pia ,aliongeza kuwa pia jeshi la polisi kwa kushirikiana na Idara ya ya
ustawi wa jamii jiji la Arusha imefanya operesheni ya kuwaondoa watoto
wadogo wanaofanya biashara mbalimbali ikiwemo kubebeshwa mizigo kati
masoko mbalimbali ya jijini hapa ambapo waliwakamata watoto 105 ambapo kati yao 46 wana umri chini ya miaka 18 na 59 wana umri wa zaidi
No comments
Post a Comment