Mahakama ya hakimu mkazi wa kisutu kutoa uamuzi dhidi ya Wabunge wa nne wa CHADEMA hapo kesho.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga kesho Jumatano Novemba 20, 2019 kutoa uamuzi dhidi ya wabunge wanne wa Chadema waliokiuka masharti ya dhamana kwa kutowasili mahakamani pasipo kutoa taarifa yoyote.
Hayo yamezungumzwa leo Jumanne Novemba 19, 2019 na hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya washtakiwa hao kumaliza kujitetea kwa nini wasifutiwe dhamana baada ya kukiuka masharti.
Hata hivyo, siku ya ijumaa novemba 15 mahakama hiyo iliamuru wabunge hao, Mchungaji Peter Msigwa; John Heche ; Halima Mdee na Ester Bulaya kukamatwa baada ya kukiuka masharti ya dhamana kwa kutofika mahakamani kusikiliza kesi ya uchochezi inayowakabili.
Aidha, Wabunge hao wamerudishwa mahabusu na kutakiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho saa 4:30 asubuhi ili mahakama hiyo itoe uamuzi dhidi ya mashtaka yanayowakabili.
Pia,amri ya kukamatwa ilitolewa na Hakimu mkazi wa kisutu Simba baada ya washtakiwa hao kutokuwepo mahakamani bila taarifa yoyote wala wadhamini wao.
Wakijieleza kwanini wasifutiwe dhamana kwa nyakati tofauti akianza Msigwa aliomba radhi kwamba haikuwa nia yake kuidharau mahakama, tangu kesi ianze hajawahi kuchelewa, hajawahi kukaidi amri ya mahakama na kwamba anaheshimu kiti cha hakimu.
Amedai ya kuwa alitokea Dodoma alidhani kesi ni saa nne na nusu kama kawaida akiwa na Heche lakini walipofika walikuta kesi imeisha na jitihada za kumuona hakimu kumaliza tatizo hilo zilishindikana.
Pia, Kwa upande wake Mdee pia ameomba radhi, ameonyesha jinsi anavyoiheshimu mahakama na kwamba alichelewa kwa kuwa alipitia kupima presha zahanati na alipofika kesi ikawa imeisha na amri imeshatolewa na wadhamini wake waliwahi lakini hawakufanikiwa kumaliza tatizo hilo Novemba 15 kwa kuwa waliambiwa amri ilishatolewa.Heche amedai aliomba asifutiwe dhamana, anadai anaheshimu mahakama, hajawahi kuidharau, siku ya kesi ilikuwa Dar es Salaam lakini alijua kama kawaida kesi yao inasikilizwa saa nne na nusu hivyo alipofika alikuta imeahirishwa.
Akijitetea Bulaya amedai Novemba 14 alienda msibani Singida kumzika mama yake mdogo lakini aliwapa taarifa wadhamini wake ambao siku ya kesi walikuwepo katika eneo la mahakama.
No comments
Post a Comment