Header Ads

Header ADS

Mkutano wa 39 wa baraza la mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki umeanza jana jijini Arusha

  Mkutano wa 39 wa baraza la mawaziri  wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umeanza jana  jijini Arusha kwa lengo la kujadili na kukubabaliana na ‘agenda’ mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo (Summit) utakaofanyika mwezi Februari, 2020.

    Mkutano huo wa siku saba umeanza leo kwa ngazi ya maofisa waandamizi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na utafuatiwa na mkutano wa Makatibu Wakuu kisha kuhitimishwa na Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo tarehe 27 na 28 Novemba, 2019.
  Pia,ajenda  nyingine za mkutano huo zinakadiriwa kuwa tisa ambazo ni pamoja na ripoti ya utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na Baraza hilo kwenye vikao vilivyopita; taarifa kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, taarifa kuhusu masuala ya miundombinu, forodha na biashara; na ripoti ya kamati ya utawala na fedha.
Hata hivyo,ajenda nyingine ni taarifa ya baraza kwa wakuu wa nchi kuhusu utekelezaji wa maamuzi/maelekezo mbalimbali yaliyotolewa kwenye mikutano ya wakuu wa nchi, na Kalenda ya Matukio ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha kuishia mwezi Juni 2019.
Pia,Ikumbukwe kuwa hadi sasa, Jumuiya ya Afrika Mashariki inaundwa na nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini.

No comments

Powered by Blogger.